Friday, August 24, 2012

BINTI WA MIAKA 15 ABAKWA NA KUNDI LA VIJANA KWENYE MELI...

Mwanaume mwenye miaka 31 ambaye ameoa ameshitakiwa baada ya binti mmoja kudaiwa kubakwa naye akiwa na kundi la vijana kwenye chumba cha meli ya kitalii ya Carnival.
Casey Dickerson alikamatwa Jumapili baada ya shambulio hilo la ngono kuripotiwa wikiendi iliyopita.
Alikana kubaka lakini akakiri kwamba aliwanunulia pombe vijana hao wakati wakipanda kwenye meli hiyo ambayo iling'oa nanga mjini Florida Agosti 16 kwa ajili ya safari ya siku nne kuelekea Bahamas.
Dickerson pia alikiri kufanya ngono na wanawake wengine ambao hawakuwa mkewe ndani ya boti.
Binti huyo, ambaye hakutajwa jina, alisema alibakwa katika chumba cha ziada ambacho Dickerson alikuwa na ufunguo wa akiba ndani ya meli.
Aliruhusiwa kutumia chumba cha pili na wafanyakazi wa meli baada ya mkewe hapo awali kulalamikia kwamba kuna kelele.
Binti huyo mwenye miaka 15 alizieleza mamlaka husika kwamba alikwenda kwenye chumba na rafiki yake mwenye miaka 15 ambako Dickerson alikuwa akisherehekea akiwa na wavulana wanne.
Binti huyo alisema walipewa pombe kabla rafiki yake kufungiwa bafuni na mmoja wa vijana huku akibakwa.
Alisema kwamba mtuhumiwa na washabuliaji wengine wakamgeukia yeye na kumwangusha chini na kuhamasishana kila mmoja kushiriki, kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana.
Kuna wakati katika shambulio hilo lililochukua muda mrefu, mtu mmoja akaingia kwenye mlango wa chumba hicho. Alikuwa amekandamizwa sakafuni wakati kijana mmoja akimfukuza mtu huyo, kwa mujibu wa taarifa.
Binti huyo alivaa nguo zake na hatimaye akaruhusiwa kuondoka chumbani humo. Alitibiwa majeraha yake katika kituo cha afya kilichomo kwenye meli hiyo ambako tukio hilo la ubakaji lilifanyika. Uongozi wa Carnival uliwataarifu FBI kuhusiana na tukio hilo.
Haikuweza kufahamika mara moja binti huyo wa miaka 15 alikuwa anasafiri na nani kwenye meli hiyo.
Vijana walidai kwa wachukunguzi wa FBI kwamba Dickerson aliwaambia wafanye mapenzi na binti huyo. Hakuna mashitaka yoyote waliyofunguliwa dhidi yao na wala hawakutajwa majina yao.
Dickerson anayetokea Casselberry, mjini Florida alisema kwamba walipanga iwe fursa ya kustarehe yeye na mkewe, akaongeza: "Meli hiyo ya kitalii yenyewe ilikuwa ya kipekee." Alidai kuwa alikuwa amelewa, kupita tu na hakufahamu chochote kwamba kuna tukio la ubakaji limefanyika chumbani.
Katika mahojiano, pale alipoulizwa kama amembaka binti, alikataa kujibu maswali zaidi. Anashikiliwa kwa tuhuma za kutenda makosa yanayohusisha ngono katika Gereza la Orange bila dhamana baada ya Jaji kumuelezea kama mtu hatari kwa jamii.
Hakuna sheria yoyote rasmi kwa matukio ya ubakaji baharini.
Ni uamuzi wa Mwanasheria Mkuu kama mashitaka ya ngono yafunguliwe dhidi ya watoto. Wakala anachunguza kesi hiyo, msemaji ameeleza.
Taarifa kutoka Kampuni ya Meli za Kitalii ya Carnival imesema: "Carnival inashirikiana kikamilifu na maofisa wa vyombo vya sheria huku uchunguzi ukiendelea."
Kumekuwa na ripoti hapo kabla za matukio ya ngono kwenye meli za kitalii za Carnival.
Novemba mwaka jana, mfanyakazi wa meli ya Carnival alituhumiwa kufanya ngono na msichana wa miaka 14 ambaye alikuwa mapumzikoni na familia yake.
Kert Clyde Jordan mwenye miaka 35 kutoka Grenada, alikuwa anafanya kazi kama mhudumu katika meli ya kitalii ya Carnival Liberty inayofanya safari zake mjini Miami. Alishitakiwa kwa kosa la kufanya ngono na mtu aliye chini ya miaka 16.
Alituhumiwa kwa kumrubuni binti huyo bafuni kwenye ghorofa ya Lido, sehemu ya juu ya boti hiyo.
Msichana aliwaeleza wazazi wake kuhusu shambulio hilo baada ya kurejea nyumbani kutoka mapumzikoni, polisi walisema.
Wakati huo, kampuni ya meli hiyo ilisema: "Carnival haina kabisa sera za kutetea matukio ya uhalifu na tunashughulikia madai yoyote kwa umakini mkubwa."
Siku kumi tu kabla ya tukio la Novemba 4, mtu mmoja wa Alabama alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa kumbaka binti wa miaka 13 ndani ya meli ya Carnival huko Mexico.
Kwa mujibu wa kumbukumbu za mahakamani, Dylan Cole mkazi wa Bloodsworth mwenye miaka 19, alikutana na binti wakati alipokuwa mapumzikoni na familia yake Machi, 2011.
Bloodsworth alimweleza binti amsindikize kwenda kuchukua jaketi chumbani kwake na kumbaka, kwa mujibu wa nyaraka za mahakama.
Meli za Carnival Sensation zinafanya kati ya safari tatu na nne kutoka Port Canaveral kwenda Bahamas. Ina uwezo wa kubeba abiria 2,056 na wafanyakazi 920. Meli hiyo inatoa huduma kwa familia kama mabwawa ya kuogelea, michezo ya kuteleza kwenye maji na klabu kadhaa za watoto.
Kampuni ya Meli za Kitalii za Carnival ina makao yake makuu mjini Miami, na ina meli 23 ambazo hufanya safari zake kwenda Bahamas, Caribbean, Mexican Riviera, Alaska, Hawaii, Canada, New England, na Bermuda.

1 comment:

Anonymous said...

Simply wish to say your article is as amazing.
The clearness in your post is just excellent
and i can assume you're an expert on this subject. Well with your permission allow me to grab your RSS feed to keep up to date with forthcoming post. Thanks a million and please carry on the enjoyable work.
Also visit my page : submit site