Wednesday, August 22, 2012

BIBI WA MIAKA 70 AMUUA MUMEWE KWA WIVU WA MAPENZI...

Kamanda wa Polisi Morogoro, Faustine Shilogile.
Ajuza mwenye umri wa miaka 70, Asha Omary mkazi wa Cha Ngedere, tarafa ya Ngerengere wilayani hapa, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji ya mumewe, Rajabu Athuman (70) kwa kinachodawa kuwa wivu wa mapenzi.
Mauaji hayo yalifanyika Agosti 19 saa tisa alasiri kijijini hapo pale mwanandoa huyo alipochukua kisu na kumchoma mumewe mkononi na kusababisha kifo chake kilichotokana na kuvuuja damu nyingi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile alisema hayo jana mjini hapa wakati akitoa taarifa ya matukio ya kuanzia Agosti 17 hadi 20.
Hata hivyo, Kamanda hakueleza kinagaubaga mazingira yaliyosababisha mwanandoa huyo kufikia uamuzi wa kumwua mumewe kwa kisu licha ya kuwapo madai ya wivu wa mapenzi. Alisema anashikiliwa kwa mahojiano zaidi.

No comments: