Thursday, August 9, 2012

BANGI SASA YAPEWA JINA LA MWANARIADHA USAIN BOLT...

Wavutaji sasa wana kila sababu ya kumshabikia Usain Bolt …si tu kwamba anatoka Jamaica …bali sasa imefahamika maduka yanayouza bangi mjini California sasa yanauza bangi iliyobatizwa jina la mtu huyo mwenye kasi zaidi duniani. Heshima gani hii...!!
Vyanzo vya habari vimeeleza kuwa tangu kuanza kwa Michezo ya Olimpiki, sehemu kadhaa zinazojihusisha na uuzaji bangi katika eneo la Orange County zimekuwa zikiuza bidhaa inayoitwa "Usain Bolt OG".
Duka moja limeeleza U.B.O.G. imepata jina lake hilo sababu "inapandisha mzuka kwa kasi sana…"

No comments: