Saturday, August 18, 2012

BABA AWAITA WAUAJI 'WAOGA', WAMTANDIKA RISASI NA KUFA...

Mtu mwenye jicho moja amekuwa mlengwa namba moja katika msako mkali wa polisi baada ya baba mwenye majonzi kuuawa kikatili ikiwa ni wiki kadhaa tu baada ya kijana wake kuuawa kwa risasi.
Polisi wamesambaza picha ya Dale Cregan mwenye miaka 29 ambaye anatafutwa kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na matukio yote mawili ya mauaji.
David Short mwenye miaka 47, alipigwa risasi nyumbani kwake huko Clayton, mjini Manchester baada ya kuwapachika jina wauaji wa kijana wake, Mark mwenye miaka 23 kwamba ni 'waoga'.
Kulikuwa na mlipuko nyumbani kwake uliosababishwa na bomu na ndani ya dakika chache kukatokea shambulio jingine la bomu na kutupiana risasi kwenye nyumba moja huko Droylsden, mashariki mwa jiji hilo.
Sasa mtu mmoja mwenye miaka 31 anashikiliwa na polisi baada ya kukamatwa kwa tuhuma za mauaji ya Mark na mashitaka mengine matatu ya kujaribu kuua. Alikuwa akishikiliwa katika Hospitali ya Wythenshawe.
Kutupiana risasi na mashambulio ya mabomu yalitokea huku watu wawili wakipandishwa kizimbani kwa mashitaka ya kifo cha Mark. Alilipuliwa na kufa wakati akicheza pool na marafiki zake kwenye klabu iliyojaa wateja.
Baba yake alipigwa risasi na kufa na watu walijifunika sura zao hatua chache kutoka sehemu walipokuwa wakicheza watoto kwenye bustani moja.
Watu hao wenye silaha walionekana wakikimbia kutoka kwenye nyumba hiyo baada ya majirani kusikia milio ya risasi.
Mmoja alisema: "Kulikuwa na milio ya risasi kati ya mitano na nane, miwili ya mwisho ilikuwa na kishindo kikubwa mno. Nilichungulia dirishani kwangu na kuona watu wawili wakikimbia huku wote wakiwa wamejifunika sura zao.
Polisi zaidi, wakiwamo wenye sialaha wamesambazwa maeneo yote mawili.
Gari jeupe, ambalo linaaminika kuhusika kwenye mashambulio yote lilizingirwa eneo la tukio kulikotokea mlipuko wa pili huko Luke Road.
Ford Fiesta ya rangi ya shaba baadaye lilizingirwa Lord Lane huko Failsworth. Magari yote yalipekuliwa na wataalamu wa kutegua mabomu kuhakikisha kuwa yalikuwa salama kwa polisi kuyakamata.
Mauaji hayo yamekuja huku Luke Livesey mwenye miaka 27, na Damien Gorman mwenye miaka 38, kuonekana kupitia video katika Mahakama ya Manchester wakisomewa mashitaka kuhusiana na kifo cha Mark, bondia wa ngumi za ridhaa.
Baba wa mtoto mmoja, alilipuliwa shingoni na kufariki papo hapo baada ya mtu mwenye bunduki kufyatua risasi kwenye baa yenye pilika ya Cotton Tree iliyoko Droylsden.
David, anayefahamika kama 'Pops' na mama wa Mark, Michelle waliwatuhumu hadharani wauaji wa kijana wao kuwa ni 'waoga' na kueleza jinsi kumbukumbu ya mauaji yake 'itakavyokaa mioyoni mwao milele".
Majirani zao walisema gari kubwa la rangi ya shaba lilionekana limeegeshwa karibu na nyumba ya familia hiyo majira ya asubuhi huku likiwa na watu wanne ndani na kujenga hofu kwamba wanajiandaa kuvamia nyumba hiyo.
Jirani mmoja alisema: "Nilikuwa kitandani na kuamka kufuatia milio ya risasi. Naweza kusema ilikuwa ni milio ya risasi."
Februari 2009, Mark alifungwa jela baada ya kumpiga na kumvunja taya muuza duka wakati huo akiwa nje kwa dhamana kwa kosa la kumpora gari mzee wa miaka 60. alihukumiwa kifungo cha miaka miwili baada ya kukiri kosa la uporaji na kujeruhi mwili.
Lakini Juni mwaka jana, Mahakama ya Rufani ilibadili adhabu hiyo na kuongeza kifungo hicho hadi miaka mitano.

No comments: