KUSHOTO: Dean na Taylor wakati wa mahojiano. KULIA: Mbakaji Jawid Armani.
Taylor Kenney alibakwa na mtu asiyefahamika miaka mitatu iliyopita akiwa na umri wa miaka 16 kufuatia ugomvi wakati walipokuwa wametoka kwa matembezi usiku mwaka 2009 na rafiki yake wa kiume Dean, ambaye baadaye akamtimua katika baa walipokuwa wakinywa pombe na kumwacha arudi mwenyewe nyumbani.
Wapenzi hao walipigiana simu muda mfupi baadaye na Taylor akaondoka kwenye baa na kukutana na Dean njiani wakati akimfuata.
Lakini binti huyo wa miaka 16 hakukutana na Dean kama walivyopanga usiku huo.
Alikuwa akifuatiliwa na mhamiaji haramu Jawid Armani ambaye alimkamata na kumkokota binti huyo kichochoroni na kumbaka.
Armani kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka sita jela kwa makosa mawili ya ubakaji na Taylor, ambaye sasa ana miaka 19, na Dean mwenye miaka 24 wamefunga ndoa na wamefanikiwa kupata mtoto wa kike, Sofia mwenye miaka miwili.
Lakini wapenzi hao, ambao wanaishi Warwickshire, wamekiri walilazimika kufanya kazi ya ziada kusahau yaliyopita na kusamehe makosa ya Dean ya kushindwa kutokea na kumlinda mpenzi wake.
Wakiongea na Ruth Langsford na Eammon Holmes kwenye kipindi cha This Morning Sofa jana, Taylor alisema:
"Tulikuwa na malumbano ya kipuuzi na Dean akaondoka kwenye baa kuelekea nyumbani.
"Kisha akagundua kuwa amefanya uamuzi wa kipumbavu.
"Nilihisi angekwenda moja kwa moja na hivyo nikaamua kuondoka na kujaribu kumfuatilia.
"Dakika kumi nikiwa njiani hakukuwa na dalili yoyote ya kumuona na hivyo ndivyo ilivyotokea.
"Sikuweza kumsikia yeyote mpaka nilipofika katika kichochoro, ndipo nikasikia kishindo cha mtu akitembea nyuma yangu na kuanza kupata mchecheto.
"Walikuwa wakija kwa kasi mno, pale nilipomaliza kichochoro akaniziba mdomo kwa mkono wake na kunivuta nyuma.
"Baadaye alinong'ona sikioni mwangu kwamba anaomba radhi, akajipukuta vumbi na kicha kutokomea tena kichochoroni."
Dean, ambaye ndio kwanza tu alikuwa ameanza urafiki na Taylor wakati shambulio hilo likitokea, alisema:
"Nilirejea kwenye baa kumtafuta lakini nikaambiwa alishaondoka.
"Nikaanza kuelekea upande mwingine na kupita kwa baadhi ya rafiki zangu ambao walisema kwamba kuna mtu ameshambuliwa lakini haikuniingia akilini.
Lakini nilipofika nyumbani na alikuwa bado hapokei simu yake nikaanza kuhisi amepatwa na matatizo."
Nashukuru kwa ushahidi wa Taylor na kidhibiti cha DNA Armani alikamatwa na kuhukumiwa kwa hili na matukio mengine ya ubakaji aliyofanya katika miezi saba kabla.
Taylor, ambaye aliamua kujitambulisha wazi kwa lengo la kuhamasisha waathirika wengine kupigania haki, aliamua kwamba hakutaka Dean ahudhurie mahakamani siku ya kusikilizwa kesi hiyo.
Alisema: "Tulisaidiana kwa kadri tulivyoweza lakini sikutaka dean aje kwa sababu nilifikiri kwamba kutakuwa na athari kubwa kwa mahusiano yetu kama angesikia kila kitu kwa undani zaidi.
"Nafikiri kwamba huo ulikuwa uamuzi mzuri sana ambao nimewahi kufanya maishani.
"Hata sasa nasumbuka kila ninapofikiria tukio lile.
"Akilini mwangu wakati mwingine huwa nafikiri "Kwanini unapita njia kama ile? Ungeweza kuwa pale na kuzuia"."
"Na katika matukio ya kuweweseka wakati mwingine naiona sura ya mbakaji kwa Dean na kumsukumia mbali, na nafahamu hicho ni kikwazo kikubwa kwake.
"Lakini amekuwa wa ajabu, amekuwa mwamba wangu, na nisingekuwa hapa nilipo bila yeye."

No comments:
Post a Comment