Mtoto wa miaka saba amefariki juzi baada ya kuanguka kutoka kwenye trela linalokokotwa na trekta linalotumia nguvu ya mvuke kwenye eneo la wazi la makumbusho.
Mtoto huyo, ambaye hakutajwa jina lake, alikuwa akifurahia kupanda kwenye gari hilo la kale ndipo ajali hiyo ikatokea.
Wafanyakazi wa huduma za dharura waliwasili kwenye makumbusho ya Beamish, karibu na Stanley, huko County Durham dakika kadhaa kabla ya saa 9 alasiri.
Mtoto huyo alipata majeraha makubwa kichwani na kufariki eneo la tukio.
Makumbusho hayo yaliyoshinda tuzo, ambayo yanahifadhi treni za umeme za abiria na mitambo mingine ya kizamani inayotembea kuzunguka viwanja vya makumbusho hayo, ilisheheni familia mbalimbali zilizofurahia mandhari nzuri na wikiendi ya kwanza ya wanafunzi walioko likizo.
Yalifungwa mara moja na kuhamishwa baada tu ya ajali kutokea.
Polisi walikataa kuthibitisha madai kwamba baba wa mtoto huyo anafanya kazi kwenye makumbusho hayo na kwamba alikuwa akiendesha gari hilo.
Dereva alikimbizwa Hospitali ya Chuo Kikuu cha North Durham na wahudumu wa huduma ya kwanza ambako alipatiwa matibabu kutokana na mshituko.
Inspekta Stephen Dowdle wa Kituo cha Polisi cha Durham alisema: "Mtoto wa miaka saba amehusika kwenye ajali ya treni linalokwenda kwa nguvu ya mvuke na trela na amethibitishwa kufariki eneo la tukio.
"Anaonekana kuwa amepata majeraha makubwa kichwani.
"Dereva wa treni alipelekwa hospitali kutokana na mshituko alioupata. Atahojiwa na polisi katika wakati mwafaka na anachukuliwa kama shuhuda wa tukio hilo.
"Utambulisho wa waliohusika haujatolewa rasmi, lakini imefahamika kwamba hakuna yeyote aliyefika kwa ajili ya kutembelea makumbusho hayo.
"Wapelelezi na maofisa wa polisi wanaosimamia sheria za barabarani wapo eneo la tukio kujua hasa kilichotokea."
Polisi walikuwa wakifanya uchunguzi wa pamoja na wakuu wa Afya na Usalama, aliongeza.
Mkurugenzi wa Makumbusho hayo Richard Evans alisema: "Tumeshitushwa mno na mawazo yetu yako pamoja na familia ya mtoto huyo kwa sasa.
Tumechukua uamuzi wa haraka kuyafunga makumbusho hayo kusaidia uchunguzi wa pamoja."
Makumbusho hayo ambayo jina lake kamili ni Living Museum of the North, yalizinduliwa katika muonekano wake wa sasa mwaka 1970 na kutunza mazingira kama yalivyokuwa mwaka 1913.

No comments:
Post a Comment