Mfuko wa hisani wa Mary J. Blige haujafanya lolote zaidi kwenye elimu ya juu, sababu baadhi ya walengwa wamefukuzwa vyuoni kufuatia Taasisi ya Mary J. Blige kuripotiwa kujiondoa katika kulipia karo.
Wanafunzi 25 ambao wamehitimu kutoka shule zote za wasichana wenye vipaji mwaka 2010 waliahidiwa ofa ya kulipiwa ada kwa miaka minne katika vyuo wapendavyo, lakini wasichana kadhaa wamesema ada zao hazijalipwa mpaka sasa.
Sarfoah, kwa mfano, anasoma chuo cha Suny Canton yumo kwenye orodha ya wanaodaiwa ada. Ameeleza taasisi hiyo ililipa kwa wakati katika mwaka wa kwanza lakini tangu wakati huo hajapokea chochote. Amelazimika kukopa na kama taasisi hiyo haitalipa mapema basi atalazimika kufukuzwa.
Mama wa msichana mwingine amesema binti yake amepitia matatizo kama hayo na amejaribu kuwasiliana na taasisi hiyo kwa njia simu na barua pepe bila kupata majibu.
Hivi karibuni immeripotiwa kwamba taasisi hiyo imeshitakiwa na Benki ya TD kwa kushindwa kulipa mkopo wa Dola za marekani 250,000.
Mary J Blige mwenyewe alikaririwa akisema kwamba watendaji wake wamemwangusha mno na kwamba anafanya kila liwezekanalo kuweka mambo sawa kwenye taasisi yake ikiwa ni pamoja kuhakikisha inalipa mkopo wa benki.

No comments:
Post a Comment