KUSHOTO: Haynes (juu) na Maureen. KULIA: Hospitali inayolalamikiwa.
Mgonjwa anayelalamikia matibabu aliyopewa yeye na mwanamke kipofu mikononi mwa nesi asiye na sifa amelibatiza tukio hilo kuwa ni ubaguzi.Sandra Hynes mwenye miaka 50 alikwenda hospitali kwa ajili ya upasuaji mdogo wa kidole tumbo, lakini kufuatia ubabaishaji akajikuta akipasuliwa pafu lake la kulia.
Alilazimika kukaa hospitalini hapo kwa wiki mbili zaidi akipumulia mashine maalumu katika jitihada za kupunguza maumivu yake.
Lakini matatizo zaidi yakazuka baada ya dripu na hewa ya oksijeni zilipoisha wakati wa wikiendi.
Cha ajabu ni kwamba, nesi wa zamu hakufundishwa jinsi ya kuchomeka sindano kwenye mkono, na pia kuhangaika kuweka oksijeni akimsababishia maumivu makali.
Alipopatiwa dawa ya morphine kienyeji, na kuanza kulia, nesi huyo alimtaka kufunga mdomo wake.
Mgonjwa wake hatimaye akashuhudia nesi akimlisha supu ya moto mgonjwa kipofu aliyelazwa kwenye kitanda cha jirani yake, akimwacha analalamika na kuugulia maumivu.
Hynes alimwambia nesi huyo ambaye alionekana ni mweusi kwamba angetakiwa kuangalia joto la supu hiyo kabla ya kumpa mgonjwa.
Baada ya matukio hayo bosi wa nesi huyo, Maureen Nwadike, ambaye naye pia ni mweusi aliingia kwenye wodi na kumweleza Haynes: "Wewe ni Mbaguzi."
Licha ya kuwa kwenye maumivu makali, mgonjwa alijaribu kuinuka na kutaka kuondoka hospitalini hapo.
Sasa, kufuatia malalamiko, Hospitali ya Chelsea and Westminster iliyoko West London imemuomba radhi kwa matibabu ya hovyo aliyopata.
Usiku wa jana Haynes anayetokea Grays mjini Essex alisema: "Niliitwa mbaguzi kwa kulalamika kuhusu msichana asiyekuwa na sifa na sababu hakukuwa na yeyote anayeweka kubadili dripu katika wikiendi yote. Ilikuwa hali mbaya sana.
"Nilikuwa katika maumivu makali, na sababu ilikuwa wikiendi hakuna yeyote ambaye angeweza kufanya chochote.
"Niliogopa kukaa wodini, na kuhusu kingeweza kutokea wakati nikiwa nimelala.
"Wakati fulani nilitafuta fimbo za kutembelea na kujaribu kutoka nje ambako ningeomba msaada mitaani.
"Sitaki kwenda tena pale, japo bado naumwa."
Kufuatia malalamiko yake, Nesi Mkuu Sian Davies amekiti kwenye barua ndefu:
"Ninakiri kwamba kuna upungufu wa madaktari siku za wikiendi, jambo ambalo husababisha kudorora kwa huduma kama ilivyotokea kwa maumivu yako, kitu ambacho hakikubaliki.
"Umefafanua pia jinsi nesi Hannah asivyojua kubadili oksijeni. Bado ni mgeni kwenye wodi, hajiamini sana, na anatumia uzoefu.
"Na umeeleza jinsi nesi Maureen Nwadike alivyokutuhumu kuwa ni mbaguzi.
"Tabia ulizoelezea haziwezi kupuuziwa na hazikubaliki. Nitafuatilia jinsi anavyowasiliana na wagonjwa."
Alipofuatwa nyumbani kwake Thamesmead, Kusini Mashariki mwa London, Maureen ambaye mumewe Atnhony mwenye miaka 54 ni Mkurugenzi wa shughuli binafsi za uuguzi, aligoma kuzungumzia suala hilo.

No comments:
Post a Comment