Monday, June 4, 2012

KUNDI LA JACKSON LAFUTA MATAMASHA MAWILI...

Kundi la muziki la Jackson limefuta matamasha yao mawili ya kwanza sababu wamekuwa bize kurekodi albamu yao mpya, imeripotiwa.
Kundi hilo lilitangaza wiki hii wamefuta maonesho yao ya mjini Louisville na Cincinnati, ambayo mwakilishi wa bendi hiyo ameeleza kuwa ni kutokana na 'kuingiliana ratiba'.
Lakini vyanzo vilivyo karibu na kundi hilo la Jackson limesema ndugu hao (Jackie, Jermaine, Marlon na Tito) wanataka kumaliza albamu kabla hawajaanza kushambulia mtaani hivyo kuweza kupiga nyimbo zao mpya kwenye ziara hiyo.
Imeelezwa kundi la Jackson linataka kufidia siku zilizofutwa lakini hadi sasa hakuna kilichopangwa.
Ziara imepangwa (ikiwezekana) kuanza Juni 20 mjini Rama, Canada.

No comments: