KUSHOTO: George. JUU: Maeneo aliyokuwa akiishi George ambapo wazazi wake hawakusikia mlio wa risasi. CHINI: Meseji yake ya mwisho wakati akichati na wenzake mtandaoni muda mfupi kabla ya kujilipua.
Kijana wa Nebraska amejipiga risasi kichwani kwa bahati mbaya wakati akiwa ameketi na bastola yake kwenye chumba cha intaneti.Watumiaji mtandao waliopigwa butwaa walionekana kutishwa mno wakati kijana huyo mwenye miaka 19, Trevor George alipoinua bastola yake na kujilipua mwenyewe Machi mwaka huu.
Baada ya uchunguzi uliochukua miezi mitatu, Polisi wa Bellevue walihitimisha Jumatatu kwamba kifo hicho cha kutisha kilikuwa ni ajali na si kujiua.
Waligundua pia, baada ya kuwahoji mashuhuda wa tukio na kupitia kumbukumbu kwenye kompyuta, kwamba George hakujaribu wala au kukusudia kujipiga risasi.
Watu kadhaa waliokuwamo katika Chumba cha Intaneti cha Tinychat ambamo George mpaka kifo chake waliieleza polisi kuwa Mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu cha Bellevue alijielekezea bastola kichwani kama masihara lakini haikuwahi kuwekwa risasi.
"Alikuwa na kawaida ya kufanya vituko kama hivi," amesema Kepteni David Stukenholtz.
"Safari hii, kwa sababu yoyote, kulikuwa na risasi kwenye chemba ya bastola ambayo haikumwachia uhai wake."
Polisi walisema wengi wa watu waliokuwamo kwenye chumba kile hawakufahamu jina halisi la George wala mahali anapoishi, na hivyo kuwa vigumu kwao kutoa taarifa ya mauaji hayo au kupiga simu kuomba msaada .
Katika mtandao wa intaneti wa kuchati, kijana huyo alikuwa akitumia majina ya TZIF na Jesus, kwa mujibu wa vyanzo vya habari.
"Hata kama ulifahamu jina lake, ungelazimika kufahamu wapi pa kupeleka msaada," Stukenholtz alisema.
Baadhi ya mashahidi waliohojiwa na polisi wanaishi Australia, Canada, Uholanzi na sehemu mbalimbali nchini Marekani.
Ajali hiyo mbaya iliripotiwa na mkazi wa Florida ambaye alikuwa akimfahamu George na alikuwa amejiunga kwenye mtandao wa intaneti kabla ya mauaji hayo.
Aliieleza polisi alijiunga tena asubuhi iliyofuata na kukuta watu wakijadili tukio hilo la kushitusha.
George alikuwa akiishi na wazazi wake katika kitongoji cha Omaha mjini Bellevue.
Wazazi wake walikuwa nyumbani wakati kijana huyo akijipiga risasi, lakini hawakusikia mlio wa risasi na hawakuwa na taarifa ya kifo cha kijana wao hadi polisi walipofika kutazama taarifa kutoka mkazi huyo wa Florida.
Watumiaji wa mtandao huo walituma meseji mbalimbali wakionesha kuchanganyikiwa baada ya mauaji hayo.
Mmoja, ambaye alijisajili kwa jina la 'Strawman' aliandika: "Nimeongea naye katika sekunde zake za mwisho. Sikugundua kama alikuwa anakufa."
Polisi wamesema George alikuwa mwanafunzi nyota na hakuonekana kama mwenye msongo ama dhamira ya kujiua.

No comments:
Post a Comment