Tuesday, June 26, 2012

HIJAB YAMSABABISHIA MAMA KUKOSA HAFLA CHUONI...

Mama mmoja amezuiwa kuhudhuria hafla ya jioni ya wazazi shuleni sababu alikuwa amevalia mavazi yaliyofunika uso wake.
Maroon Rafique mwenye miaka 40, alielezwa kwa ulinzi na usalama wa watoto na walimu katika chuo kuna amri ya kupiga marufuku mavazi yanayoziba sura.
Alitahadharishwa kwama isipokuwa tu akiondoa vazi hilo linaloziba uso maarufu kama hijab, ndipo angeruhusiwa kuingia chuoni humo kuhudhuria hafla hiyo.
Mwishowe, Maroon akiwa amefadhaika akalazimika kumpigia mumewe aliyekuja kuchukua nafasi yake akiingia na mtoto wao wa kiume, Awais mwenye miaka 18.
Maroon ambaye amekuwa akivaa hijab kwa miaka saba alisema: "Nimezaliwa katika nchi hiina Mwingereza. Kwanini kwa mavazi yangu nimkwaze mwingine? Sihitaji kuleta msukosuko wowote. Nilichotaka ni kuja kupata taarifa zitakazomsaidia kijana wangu kwenda chuo kikuu.
"Ningeruhusiwa kukaa nyuma au mbele, popote ambako nisingeweza kuonekana, kama walifikiri ningemkwaza yeyote.
"Nimesikitishwa mno sababu wakati wote nilipofika chuoni hapo kabla hakukuwa na matatizo yoyote, isitoshe wahadhiri wamekuwa wakinikaribisha vizuri na kirafiki."
Maroon anayeishi Whalley Range mjini Manchester, alikuwa amealikwa kuhudhuria siku ya wazazi jioni na kuzungumzia elimu ya vijana wao kwenye Chuo cha Manchester.
Lakini pale mama huyo wa watoto wawili alipowasili alizuiwa na walinzi kwenye lango la kuingilia chuoni hapo Kampasi ya Northenden.
Maroon ambaye ameolewa na Abdul mwenye miaka 40, na ambaye ana mtoto mdogo wa kiume Ibrahim mwenye miaka 12, anahisi kuumizwa sana.
Aliongeza: "Nimekuwa nikidhalilishwa kila mara na tena mitaani, ambacho nimekuwa nikishughulikia. Hatahivyo, nilishangazwa mno pale nilipofanyiwa hivi na chuo."
Mwanafunzi wa masomo ya Biashara, Awais mwenye miaka 18, ambaye anamatumaini ya kusomea Uhasibu katika Chuo Kikuu cha Manchester alisema: "Hakika ilikuwa inakera sana pale walipomwambia hawezi kuingia ndani. Hatujawahi, kamwe kuelezwa kuhusu sheria ya jinsi wazazi wanavyotakiwa kuvaa."
Msemaji wa Chuo cha Manchester alisema suala la Maroon limechukuliwa kwa 'uzito wa hali ya juu' kufuatia kilichotokea.

No comments: