Monday, June 25, 2012

CHEKA TARATIBU...

Mlokole mmoja kazingirwa na mafuriko makubwa nyumbani kwake maeneo ya Bonde la Jangwani. Mara akatokea jamaa na boti yake akamwambia, "Ingia twende ndugu yangu!" Mlokole akajibu, "Hapana, nina imani Mungu atatenda muujiza wake." Wakati maji yakiongezeka akatokea jamaa mwingine na boti akamwambia, "Mtumishi panda tuondoke!" Mlokole akaendelea na msimamo wake kusubiria miujiza ya Mungu. Maji yalipofikia kichwani ikatokea helikopta na kumshushia kamba wakitaka ashikilie wamuokoe, lakini Mlokole akagoma kabisa akidai kusubiri muujiza. Mwishowe mlokole akafa na moja kwa moja akakutana na Mtume Petro katika geti la kuingia peponi. Bila kuchelewa akaeleza masikitiko yake, "Niliamini Mungu atanitendea muujiza lakini nasikitika sana kwamba ameniangusha!" Mtume Petro akamjibu, "Sielewi unalalamikia nini, tumekutumia boti mbili na helikopta!" Ebo...

No comments: