Tuesday, June 5, 2012

CHEKA TARATIBU...

Wanasiasa watatu kutoka vyama vya CCM, CHADEMA na CUF wanasafiri kwenye boti maalumu katika Ziwa Viktoria. Mara boti yao ikaanza kuingiza maji na kuelekea kuzama. Jaketi la kujiokoa liko moja. Ndipo jamaa wa CUF akatoa wazo kuwa ipigwe kura nani achukue jaketi. Basi wakaamua kupiga kura kwa kuandika kwenye kipande cha karatasi na kutumbukiza katika kopo. Ikafika wakati wa kuhesabu kura. CUF na CHADEMA wakapata kura moja kila mmoja. CCM akaibuka na kura nane! Duh! Ama kweli siasa noma…

No comments: