Monday, June 4, 2012

BAKTERIA WA AJABU WANAOKULA NYAMA MBICHI WAMSHAMBULIA BINTI...

Aimee akiwa katika picha tofauti alizopiga kabla ya maambukizi hayo.
Msichana anakabiliwa na maambukizi ya bakteria wanaokula nyama mbichi na sasa yuko katika hali mbaya sana kwenye Hospitali ya Augusta.
Aimee Copeland viganja vyake vyote viwili na mguu wake vimekatwa katika upasuaji mkubwa hivi karibuni.
Madaktari wa upasuaji hapo kabla walilazimika kukata mguu wa msichana huyo mwenye miaka 24 sehemu ya pajani.
"Ninachoweza kusema ni kwamba Aimee yuko katika hali mbaya," msemaji wa hospitali hiyo Barclay Bisho alieleza.
Sala na meseji za kumpa moyo zimeendelea kumiminika kwa Aimee katika mtandao wa Facebook ambako baba yake, Andy Copeland amekuwa akimhangaikia binti yake.
Jarida moja la Atlanta limesema familia imezidiwa na hamu ya wananchi kutaka kujua kinachoendelea na hivyo wameomba unyeti katika kipindi hiki.
Wakati Aimee alipogundua kwamba angepoteza mikono yake na mguu uliobaki, alijibu kwa kusema, "Acheni wafanye hivyo".
Baba wa Aimee aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kigugumizi alichopata kuongea na binti yake siku moja kabla ya binti yake kupata bakteria hao baada ya ajali.
Alisema 'hakutokwa machozi, hakupepesa kabisa kope. Nilikuwa nikilia sababu mimi ni baba mwenye fahari ya kuwa na binti jasiri mwenye hamasa", alisema Andy Copeland kwenye meseji yake.
Aimee anasumbuliwa na jereha kubwa mguuni baada ya kuanguka Mei Mosi wakati akivuka Mto Georgia, na bakteria hao hatari kuingia mwilini kupitia kwenye jeraha hilo.
Baba yake alisema kwamba mwishowe aliweza kumweleza binti yake siku kadhaa baadaye kilichotokea baada ya matembezi na jinsi gani atarajie mapenzi kutoka kote duniani.
"Tulimwambia kwamba dunia inampenda na kumkubali," aliandika baba huyo. "Tulifafanua kuwa amekuwa ishara ya matumaini, upendo na imani."
Alikumbukia jinsi macho ya Aimee yalivyopanuka, sura yake kushuka. Kisha, Andy kuchukua mkono wa binti yake na kuiinua mpaka usawa wa uso wake.
"Hakuonesha kutishika. Alijua hali aliyomo," aliandika.
Alielezea kwamba madaktari wanaamini viganja vyake vilikuwa vikizuia maendeleo yake, na ililazimika kuondolewa. Aimee aliinamisha kichwa, baba yake alisema.
"Alitabasamu na kuinua mikono yake juu, kwa umakini akaichunguza," aliandika baba yake.
"Kisha akatutazama. Wote tulielewa maneno yake matatu yatakayofuata, 'Acha tufanye hivyo'."
Mwanafunzi huyo mwenye miaka 24 kutoka kitongoji cha Atlanta bado yuko katika hali mbaya wakati akipambana na maambukizi yanayofahamika kitaalamu kama 'necrotizing fasciitis'.
Madaktari wanaamini kuwa wangeweza kuokoa mguu wake uliobakia baada ya siku mbili za matibabu wakitumia chemba ya hali ya juu zaidi, ambapo mgonjwa hupumua kwa kutumia oksijeni halisi kuinua chembe nyeupe za damu na kuongeza kasi ya uponyaji.
Lakini baadaye wakagundua kwamba lazima wakate mguu na vidole vyake.
Bakteria wanaokula nyama mbichi, Aeromonas hydrophila huacha sumu ambayo hukatisha mzunguko wa damu kwenda maeneo mbalimbali ya mwili. Mashara yake ni kuharibu misuli, mafuta na vimelea vinavyounda ngozi.
Wiki kadhaa tu zilizopita, madaktari walimpatia fursa kidogo ya kuishi. Lakini siku za hivi karibuni ametahadharishwa na kwamba amekata tamaa vya kutosha kiasi cha kuagiza kitabu ajisomee.
Madaktari walilazimika kukata sehemu kubwa ya mguu wake wa kushoto ili kuokoa maisha yake.
Amekuwa hawezi kuongea sababu ya njia yake ya kupumulia katika koo, lakini wazazi wake wameweza kugundua midomo uake na sasa wanaweza kuwasiliana na binti yao, ambaye pia alikuwa akiagiza aletewe ice-cream.
"Madaktari wameshindwa kutoa sababu za kuimarika kwa afya yake hivi alivyo," alisema Andy.
"Roho yake ni ya kipekee kabisa. Nimeshangazwa mno."
Alimalizia kuwa binti yake anaonesha kwamba anajua kwamba yuko hospitalini baada ya ajali. Lakini kwa sasa, wamemficha taarifa zote kuhusu hali yake hadi hapo atakapotoka kwenye mashine na kuanza kupumua mwenyewe.

No comments: