Wednesday, June 6, 2012

BABA WA MEL GIBSON NAYE ADAI TALAKA...

KUSHOTO: Mel Gibson na mkewe, Robyn. KULIA: Hutton Gibson.
Kijana wake, Mel aliishangaza dunia pale aliposhikilia rekodi ya kuwa miongoni mwa watu waliolipa fidia kubwa kama malipo ya madai ya talaka kutoka kwa mkewe Robyn na pia alipositisha mahusiano na rafiki yake wa kike, Oksana Grigorieva.
Na sasa, akiwa na miaka 93, Hutton Gibson anadai talaka kutoka kwa mkewe, Teddy Joye Gibson baada ya miaka 10 ya ndoa yao.
Pingamizi Kanisani limebainisha tofauti zisizoweza kurekebishika kuwa ni sababu ya kutengana na Joye, ambaye anasemekana kuwa na miaka 70.
Wawili hao walioana mwaka 2002, miaka miwili baada ya kifo cha mama wa Mel ambaye ni mke wa kwanza wa Hutton, Anne.
Hutton na Anne walifanikiwa kupata watoto 11 ambao sasa wamemfanya awe na wajukuu 50.
Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, Hutton amemtaka mke huyo kulipa gharama zote za kesi pia anataka apatiwe msaada matunzo.
Wakili wa Hutton, Fahi Hallin amesema: "Ninatumaini takala itaisha salama. Siko tayari kwa sasa kuzungumzia sababu za mteja wangu kuamua kudai talaka, au kwanini anadai msaada wa matunzo."

No comments: