"Nimesikia una mbwa amepewa jina la Oprah ... hiyo haikuwa sifa," alisema Oprah.
Kwa aibu akajibu, "Nakupenda ... unafahamu jinsi gani wanasema mbwa ni rafiki mkubwa wa binadamu?"
Wakati wa makabiliano hayo, sehemu ya Shoo mpya ya Oprah, "Next Chapter," ... 50 Cent alielezea jinsi alivyojisikia kuhusu kampeni maarufu ya Oprah dhidi ya N-word na kushushwa daraja wanawake kwenye hip hop kuhisi kama shambulio binafsi.
"Niliweza kuona matukio kadhaa wakati unapojadili hisia zako katika utamaduni, na kila kitu pale kilikuwa kinyume na utamaduni uliokuwamo kwenye CD yangu ... na nilijihisi kama 'huyu mwanamke hanipendi.'"
Hivyo kwanini nikamwita mbwa Oprah? 50 Cent alimweleza Oprah, "Wakati huo, nilikuwa nikijaribu kutazama tukio lenyewe na nikaona naendelea hisia hasi kwa mtu ambaye hata hanifahamu."
50 Cent alisema pia anaye paka ... na kampa jina la Gayle.
Lakini sasa, tofauti zinaonekana zimezikwa rasmi.
No comments:
Post a Comment