Nyumba walimokuwa ambayo ilishika moto na kukatisha uhai wa watoto sita kwa mpigo iliyoko Allenton mjini Derby.
Moto ulioua watoto ndugu sita wakike na kiume ambao ni ndugu waliokuwa wamelala kitandani uliwashwa kwa makusudi, polisi wanaamini hivyo.Jade Philpott mwenye miaka 10, John miaka 9, Jack miaka 7, Jessie miaka 6, Jayden miaka mitano na Duwayne miaka 13 walifariki baada ya moto kuzuka ndani ya nyumba yao iliyoko Allenton, mjini Derby mapema alfajiri.
Msaidizi wa Polisi Konstebo Syeve Cotterill alisema: "Baada ya uchunguzi wa kinantunaamini moto huo haikuwa bahati mbaya, dalili za mwanzo zinaonesha uliwashwa kwa makusudi na kusababisha vifo vya watoto hao."
Duwayne amekuwa mtoto wa sita kufa baada ya mashine yake ya kupumulia kuzimwa mapema asubuhi, wakati wazazi wake Mick Philpott mwenye miaka 54 na mkewe, Mairead mwenye miaka 31 wakiwa wameketi kando ya kitanda chake.
Mtoto huyo alipelekwa kwa wataalamu wa majeraha ya moto baada ya kuokolewa kutoka kwenye moto uliokuwa ukiwaka katika nyumba yao yenye vyumba vitatu.
Polisi wamesema kwamba Duwayne alifariki kwenye Hospitali ya Watoto ya Birmingham.
Mchana huu ilithibitika kwamba uchunguzi umegundua kwamba waathirika wote watano wa moto huo wamekufa kutokana na madhara ya moshi.
Cotterill alisema: "Nina huzuni kuthibitisha kwamba Duwayne amefariki kutokana na majeraha ya moto aliyokuwa nayo.
"Rambirambi zangu ziwaendee Bwana na Bibi Philpott katika kipindi hiki kigumu.
"Inaeleweka Bibi Philpott alikuwa na Duwayne hapo kabla ya kukutana na mumewe, lakini Bwana Philpott, mfanyakazi wa zamani wa bekari, alimlea kama mwanae wa kumzaa mpaka hivi leo.
Bwana Philpott, baba wa watoto 17, kati yao watano wa kike, alijaribu kila awezalo kuwaokoa watoto wote, polisi wamesema.
Mpenzi wake wa zamani, Lisa Willis mwenye miaka 28, na shemeji yake, Ian Cousins walikamatwa kwa tuhuma za mauaji lakini wakaachiwa baadaye bila kufunguliwa mashitaka.
Cotterill alizungumza mapema kushangazwa na kitendo cha kukosa ushirikiano wa taarifa za tukio hilo kutoka kwa jamii.
Alisema: "Wakati nikiwashukuru wanajamii tulioshirikiana nao, nashangazwa kwa uchache wa watu waliokuja kutupa taarifa. Kwa kawaida kesi kama hizi taarifa nyingi hutufikia polisi kuhusu kilichotokea.
"Nahisi kuna mmoja wenu katika jamii anayefahamu zaidi kuliko haya tulivyoelezwa."
Mpaka walipotengana mwezi Februari, Bi Willis na watoto wake watano walikuwa wakiishi kwenye nyumba hiyo iliyoteketea moto hapo Allenton, mjini Derby.
Watoto wanne walikuwa wa Bwana Philpott, japo alikuwa akimlea mtoto mkubwa wa Willis aliyemzaa kwenye mahusiano yake ya awali, Jordan mwenye miaka 12. Inaeleweka kwamba aliwachukua watoto hao wakati walipotengana.
Bi Willis wakati huo alikuwa akiishi na Cousins na dada yake Amanda mwenye miaka 37.

No comments:
Post a Comment