Meya wa Jiji la Oslo amezindua uchunguzi kuhusu tamasha la mwimbaji Justin Bieber nchini Norway usiku wa kuamkia leo ambapo wasichana 49 walijeruhiwa kwenye msongamano mkubwa na 14 kati wakachukuliwa kwa gari la wagonjwa kukimbizwa hospitali kupatiwa huduma ya dharura.
Hakuna aliyeumia vibaya sana, lakini Meya Fabian Stang alisisitiza, "Nimeagiza Taasisi ya Mipango ya Dharura kuchunguza tamasha zima kuanzia mpangilio wa jukwaa hadi uwezeshaji wa tamasha hilo. Tunatakiwa kujua wapi kulikuwa na dosari na kwanini hili likatokea."
Meya Stang alisema hali ilikuwa mbaya sana, alilazimika kujificha kwenye moja ya miti wakati fulani kukwepa madhara.
Baadhi ya watu walilazimika kutumia kila njia kuweza kufika kwenye jukwaa.

No comments:
Post a Comment