Mamlaka za usalama nchini Venezuela zinawasaka vibaka waliovunja chumba cha hoteli alimopanga mwimbaji gwiji wa Hispania, Julio Iglesias na kumwibia kila kitu wakati mwimbaji huyo akitumbuiza kwenye tamasha wiki hii.
Kwa mujibu wa maofisa wa Venezuela, vijana wabaya walitokomea na fedha taslimu Dola za Marekani 1,600, iPad tatu na sanduku dogo lililokuwa na kamera ya video, kompyuta na nyaraka binafsi.
Maofisa wamesema wapelelezi wanawahoji wafanyakazi wa hoteli hiyo na kuna matumaini ya picha za kamera za usalama hotelini hapo zitasaidia kutambua yeyote aliyeiba vitu vya gwiji huyo wa muziki.

No comments:
Post a Comment