Lakini wamiliki wa nyumba moja kufanya hivyo ni jambo la kawaida sana kila mara waingiapo msalani.
Picha zinaonesha bafu la nyumba moja mpya ambayo ipo ghorofa ya 15 kwenye jengo hilo ikiwa imejengwa kwenye njia ya lifti ambayo kwa sasa haitumiki.
Wakati wamiliki hao wakifanya shughuli zao za kawaida asubuhi mjengoni humo, kama kutumia choo au kupiga mswaki, wanaweza kuona chini kupitia sakafu ya kioo hadi chini kabisa ya shimo hilo lililokuwa likitumika kwa ajili ya lifti.
Nyumba hiyo ya kifahari ipo kwenye ghorofa ya juu katika jengo lililokuwa likitumiwa enzi za ukoloni miaka ya 1970 nchini Mexico. Nyumba hiyo ni ubunifu wa kampuni ya uhandisi Hernandez Silva Arquitectors.
Kwa mujibu wa taarifa, wahandisi wamesema: "Imetokea tu kwamba sehemu ambayo hapo kabla ilikuwa iwekwe lifti ya pili haikuwekwa, sasa imekuwa sehemu ya kujirembea ikiwa na sakafu ya kioo ambapo mtu anaweza kuona chini kutokea ghorofa ya 15.
"Ubunifu huo umetumia kioo na malighafi nyingine nyingi rahisi na nyepesi."

No comments:
Post a Comment