Friday, May 4, 2012

OFISI ZA TYLER PERRY ZATEKETEA MOTO...

Himaya ya Tyler Perry inateketea, na si kwa njia nzuri, jengo ilipo studio yake Atlanta ambapo filamu zake maarufu za 'Madea' zinatengenezewa zimenaswa zikiteketea moto.
Kwa mujibu wa taarifa, vifaa vitatu maalumu vya kugundua hatari ya moto vilivunjika kwenye studio ya Tyler Perry muda mfupi kabla ya saa 3 usiku na upande mmoja wa jengo hilo umeanguka.
Studio hizo zipo kwenye eneo lenye ukubwa wa ekari 60 za ardhi ambazo zinajumuisha majukwaa, sehemu ya kubadilishia nguo pamoja na ofisi za Perry.
Hakuna taarifa zozote za majeruhi wala chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

No comments: