Tuesday, May 22, 2012

NUSURA MBWA WAMTOE ROHO UFUKWENI...

Mwanaume mmoja anapigania maisha yake akiwa hospitalini baada ya kung;atwa na mbwa wawili ufukweni.
Mtu huyo ambaye hakutajwa jina mwenye miaka 30, aling'atwa sehemu mbalimbali mwilini mwake na mbwa hatari kwenye ufukwe wa Brighton, East Sussex Ijumaa iliyopita majira ya asubuhi.
Mzee mmoja mwenye miaka 40 anayeaminika kumiliki mbwa hao alikamatwa eneo la tukio akituhumiwa kwa makosa ya shambulio na kumiliki kisu na dawa za kulevya Daraja A.
Mbwa hao hatari waliendelea kumshambulia mwanaume huyo hata alipojaribu kujitetea kukwepa majeraha zaidi.
Polisi na madaktari wasio na mipaka walishindwa kufika eneo la tukio kwa hofu kwamba na wao wangeshambuliwa pia.
Polisi wenye silaha na askari wa kikosi cha mbwa wakalazimika kuitwa eneo la tukio, jirani na eneo maarufu mjini humo la Palace Pier. Polisi mmoja alijeruhiwa mkononi na mguuni wakati akijaribu kuwakabili mbwa hao.
Shuhuda wa tukio hilo, Jack Le-Flay mwenye miaka 20 alisema: "Nilikuwa nikirejea nyumbani baada ya mayembezi ya usiku ndipo nikaona shambulio hilo. Tuliweza kuona mbwa hawa wawili wakikokota kitu fulani kutoka kwenye maji.
"Mwanzoni tulidhani lazima yatakuwa zoezi la mafunzo ya polisi au gurudumu la zamani lakini baadaye tuliweza kuona mguu.
"Mbwa walimkimbilia mmiliki wao na kisha kurejea na kuanza kumshambulia tena mtu yule. Kulikuwa na damu kuzunguka midomo ya mbwa hao.
"Mtu huyo alikuwa ametapakaa damu huku akiwa amelala uso chini kwenye maji. Sijawahi hapo kabla kushuhudia mbwa wakifanya vitu kama vile."
Mbwa hao kwa sasa wamehifadhiwa mahalim maalumu wakati polisi wakichunguza tukio hilo.
Hali ya mwanaume huyo ni mbaya lakini anaendelea kuimarika na amelazwa kwenye hospitali jirani ya Royal Sussex County.
Inspekta Mpelelezi Ian Still kutoka Ofisi ya Upelelezi yaBrighton na Hove amesema: "Linaonekana ni tukio baya sana. Bado tupo kwenye hatua za mwanzo za uchunguzi wetu.
"Bado tunajaribu kufanyia kazi kwa nini tukio hili limetokea. Mbwa bado walikuwa wakiendelea kumshambulia mtu yule hata baada ya polisi kuwasili na maofisa hawakuweza kumfikia mtu huyo mwanzoni."

No comments: