Sunday, May 27, 2012

MWANAMKE ANAYEDAIWA KUFANYA NGONO KWENYE TEKSI ATIMULIWA KAZI...

Rebecca akitoka kwenye jengo alimokuwa akifanyia kazi huku akiwa kabeba boksi lenye vitu vyake baada ya kutimuliwa kazi.
Mfanyabiashara wa Uingereza anayetuhumiwa kufanya ngono kwenye teksi huku akiwa amelewa chakari mjini Dubai, amefukuzwa kazi.
Rebecca Blake mwenye miaka 29 ametimuliwa baada ya kuamriwa na bosi wake aliyechukizwa na kashfa hiyo kupakia kila kilicho chake kutoka ofisi hizo za kampuni inajojihusisha na masuala ya ajira ya Manpower Professional.
Aliongea huku akibubujikwa machozi katika simu yake ya mkononi wakati akitoka makao makuu ya kampuni hiyo akiwa amebeba ubavuni boksi lililokuwa na vitu vyake.
Rebecca anayetokea Croydon, kusini mwa London na fundi uchomeaji vyuma kutoka Ireland, Conor McRedmond walikamatwa mapema mwezi huu baada ya kutumia siku nzima kunywa pombe.
Wawili hao walishikiliwa kwa siku tano na kushitakiwa kwa kutembea nje ya ndoa na kunywa pombe hadharani ambapo yote hayo ni makosa ya jinai katika mamlaka hiyo inayoongozwa kwa sheria kali za Kiislamu.
Rebecca, aliyeajiriwa kwa muda na Max Clifford, atakabiliwa na kifungo cha hadi miaka mitatu jela kama atapatikana na hatia. Alikana mashitaka yote.
Ofisi ya Clifford imethibitisha kwamba ametimuliwa kazi.
Rebecca, mshauri wa mambo ya ajira, alikutana na McRedmond kwenye Hoteli ya Kijiji cha Ireland ambapo wateja hulipia Pauni za Kiingereza 10 kwa ajili ya promosheni ya kunywa uwezavyo siku nzima.
Baada ya kunywa kwa masaa 12, wawili hao walichukua teksi kuelekea Dubai Marina.
Dakika baadaye walinaswa na dereva wa teksi kupitia vioo vya gari wakiwa katika hali ya kufanya mapenzi, kwa mujibu wa ripoti za polisi.
Kufuatia kukerwa na tabia hiyo, dereva huyo akasimamisha gari na kwenda kuwaripoti kwa polisi wa doria aliyekuwa kwenye gari lililoegeshwa jirani.
Aliporejea akiongozana na polisi, wakawaona Rebecca na McRedmond wakifanya ngono kwenye kiti cha nyuma cha teksi hiyo, imedaiwa.
Vyanzo vya habari zimesema: "Walikuwa wamelewa chakari, wakaanza kubusiana na kukumbatiana. Kisha wakaanza kufanya ngono.
"Polisia aliwafuata kwenye gari, alikuta mwanamke akiwa mtupu na walikuwa wakifanya ngono kwenye kiti cha nyuma."
Baada ya kukamatwa kwao, wawili hao walipelekwa kwenye kituo cha polisi cha jirani cha Jebel ali na kuwekwa rumande kutoka Mei 4 hadi Mei 9, mwaka huu.
Polisi waliwachukua kipimo cha DNA kama ushahidi kwamba walikuwa wakifanya ngono na kwamba walikuwa wamelewa.
Polisi wanangojea majibu ya kipimo hicho kutoka maabara ya mkemia mkuu kabla ya kuwafikisha wawili hao mahakamani.

No comments: