Thursday, May 3, 2012

MUUAJI HATARI WA WATU WAWILI ANASWA...

Colin Dunford (kushoto), James Allen na Julie Davison (kulia).
Mwanaume aliyekuwa akisakwa nchi nzima kwa tuhuma za mauaji ya watu wawili majumbani kwao amekamatwa.
James Allen mwenye miaka 36 alikamatwa kusini mwa mji wa Leeds akihusishwa na vifo vya Colin Dunford mjini Middlesbrough, na Julie Davison mjini Whitby.
Mpango huo ulifanikiwa baada ya kikosi cha tatu cha polisi kuhusishwa katika msako kufuatia fununu za kuonekana muuaji huyo mjini Leeds wakati wa mchana.
Msemaji wa Polisi wa West Yorkshire alisema allen alikamatwa katika Barabara ya Crown Point baada ya ofisa wa polisi aliyekuwa mapumzikoni kumwona mtu anayeendana na taarifa alizonazo za mtuhumiwa huyo.
Mkuu wa Polisi msaidizi Konstebo Mark Milsom wa Kituo cha Polisi cha West Yorkshire alisema: "Ofisa aliyekuwa mapumzikoni akisafiri kuelekea kazini asubuhi alimwona mtu anayeendana na taarifa za Jmes Allen katika Barabara ya Crown Point mjini Leeds.
"Akaita wenzake kumsaidia ambao walifika haraka sana na kumkamata mtuhumiwa.
"Tunapenda kuwashukuru washirika wote wa jamii ambao walikuwa wakiwasiliana nasi kufanikisha jambo hili."
Amri ya msako kumtafuta Allen ilitolewa na Kituo cha Polisi cha Cleveland na cha North Yorkshire kufuatia mauaji ya Bi Davison mwenye miaka 50 na Dunford mwenye miaka 81.
Polisi wa West Yorkshire waliungana kwenye msako baada ya Allen kuonaswa kwenye kamera za CCTV akitembea kando ya Barabara ya Harehills majira ya saa 8 mchana.
Hadi muda huo ilikuwa inawezekana kabisa kwamba Allen alikuwa tayari amekwenda sehemu nyingine na hivyo polisi wakatoa wito kwa yeyote atakayemuona kupiga simu polisi kwa namba 999.
Polisi walisema Allen alichukuliwa kama ni hatari na wananchi wakatahadharishwa kutokabiliana naye, ila kuwasiliana na polisi mara moja.
Polisi pia wakatoa hadharani picha za Allen zilizonaswa na CCTV mjini Scarborough mapema wiki iliyopita.
Picha hizo zilionesha allen akibadilisha fedha kwenye duka moja Jumanne iliyopita na Jumatano katika duka lake la vifaa vya michezo.
Inasemekana kuwa pengine allen alikuwa akijaribu kubadili muonekano wake kwa kurefusha nwele zake.
Polisi walithibisha kuwa Allen alionekana akipata kifungua kinywa huku akiwa kitandani katika inayohisiwa kuwa ni Hoteli ya Allerton Croft mjini Scarborough, usiku wa Jumatano iliyopita.
Mpelelezi mmoja alisema Polisi wa Cleveland wamekuwa akipokea mamia ya simu kutoka kwa raia wema kufuatia wito wa kutaka mwenye taarifa zozote kuhusu Allen ama yeyote aliyempangisha kuwasiliana na polisi haraka.
"Hakuna muda wa kulindana. Haiwezekani kupata muda huo katika kipindi kama hiki. Huu ni wakati wa kuisaidia polisi," alisema. "Sasa ni wakati wa kuwa na moyo wa kizalendo."
Inspekta Lang ametoa wito kwa Allen kujikabidhi mwenyewe: "Jitoe mwenyewe. Jitoe mwenyewe sasa.
"Unatakiwa kuwa chini ya uangalizi wa polisi, unajua unatakiwa kuwa chini ya uangalizi wa polisi, unajua ulichofanya.
"Nafikiri kiuhalisi na kwa urahisi kwa matukio haya ya kutisha yaliyofichuliwa, huyu mtu anahitajika kukamatwa na hii inatakiwa kufanyika haraka iwezekanavyo."
Inspekta huyo akatahadharisha wakazi kuweka salama nyumba zao na kuwa makini kukaribisha watu wanaobisha milangoni mwao.
Dunford ambaye alionekana akiwa hai kwa mara ya mwisho Jumapili iliyopita, alikutwa amekufa huku akiwa na majeraha makubwa kichwani nyumbani kwake Mtaa wa Leven, Middlesbrough siku iliyofuatia baada ya kushindwa kuhudhuria kwenye klabu ya Samuelsons aliyokuwa na mazoea ya kwenda kila siku. Wapelelezi wamesema hakukuwa na dalili zozote za mtu kuingia kwa nguvu kwenye nyumba hiyo.
Bi Davison, aliyekuwa akiishi peke yake, alikutwa amekufa kando ya dada yake kwenye ghorofa alimopanga eneo la Church Square Jumatano iliyopita. Naye pia alikuwa na majeraha makubwa kichwani, walisema polisi.

No comments: