JUU: Eduard Mereohra (kushoto). KATIKATI: Wastaafu David na Dorothy Metcalf enzi ya uhai wao. CHINI: Eneo la ajali ambapo gari la wastaafu hao likiwa nyang'anyang'a (lenye rangi ya bluu). KULIA: Mtoto wa wastaafu hao, Clive Metcalf.
Familia ya wanandoa waliouawa na mhamiaji haramu aliyekuwa akiendesha gari huku amelewa imelaumu mamlaka za Uingereza zinazohusika na ulinzi wa mipaka.Mhamiaji Eduard Mereohra mwenye miaka 26 alifukuzwa nchini humo mwaka 2009 lakini akarejea tena miezi michache baadaye.
Katika sherehe moja ya Mwaka Mpya, alikuwa akinywa pombe kwenye sherehe siku moja kabla ya kulibamiza gari lake kwenye gari lililobeba wazee David na Dorothy Metcalf na kuwaua wote na kutenganisha familia hiyo kwa vilio.
Juzi, baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka tisa jela, familia ya wanandoa hao ilisema wangekuwa bado wako hai sasa kama mfumo wa uhamiaji usingewaangusha.
Wamewataka maofisa kuchunguza jinsi gani raia huyo wa Moldova aliweza kukwepa mamlaka husika mipakani.
Mahakama imeelezwa kwamba Meheohra hakuwahi kupata kibali cha kufanya kazi wala namba ya bima ya taifa kwa jina lake halisi, lakini usiku wa jana yake hii ikafahamika kwa Wizara ya Mambo ya Ndani na Idara ya Kazi na Pensheni.
Nje ya Mahakama, kijana wa wanandoa hao Clive alisema: "Mama na Baba walikuwa wachapakazi, walipakodi waaminifu waliojipanga vizuri kwa kustaafu kwao na wangeweza kuwa na miaka 20 zaidi ya kuburudika pamoja.
"Wakati tukimshikilia Mereohra kutokana na kuhusika na tukio hili, tunahisi kwamba mama yetu na baba wangekuwa hai leo kama mfumo usingeshindwa kwa kumruhusu mtuhumiwa kuingia Uingereza.
"Tulikuwa karibu sana na familia na tumepotea bila wao. Hakuna hukumu inayoweza kutosha kwa mtu aliyebadilisha maisha yetu milele katika Siku ya Mwaka mpya 2012, alipochukua uhai wa wazazi wetu na mababu wa watoto zetu, kupitia kukosa fikra, hatari na vitendo vya uvunjaji sheria."
Meheohra aliwasili Uingereza Oktoba 2008, na kuomba uraia mwaka uliofuata. Maombi yake yalikataliwa na kurejeshwa Austria, ambako baadaye aliomba uraia Desemba 2009.
Lakini Aprili 2010 alireudi kwa njia za panya nchini humo kwenye lori lililokuwa likiendeshwa na raia wa Romania.
Wakati wa ajali alikuwa akiishi Burley, mjini Leeds na kufanya kazi kama kibarua. Siku ya Mwaka Mpya, alikunywa bia, wiski na shampeni kwenye tafrija usiku wa kuamkia siku ya ajali, akiendesha gari lake aina ya Volvo C70.
Mashabidi wamemuelezea alikuwa akiendesha kwa spidi kubwa kwenye barabara kuu nje ya Leeds, kwa fujo akilazimisha magari mengine yampishe njia.
Akaishia kujibamiza nyuma ya gari la Metcalf aina ya Fiat Panda akiwa kwenye mwendokasi unaofikia kilometa 100 kwa saa na kuruka juu umbali wa futi 10 kabla ya kutua chini kwa kishindo.
Bwana Metcalf mwenye miaka 68 kutoka Leeds aliyekuwa akiendesha, alitupwa nje ya gari na kufa papo hapo. Mkewe mwenye miaka 65 alikutwa akining'inia kwenye dirisha la nyuma na lifariki baadaye.
Mereohra aliyekuwa âmelewa mara mbili ya kiwango kinachoruhusiwa, alijaribu kukimbia lakini akadhibitiwa na watu waliokuwa jirani.
Baadaye alijaribu kulaumu tukio hilo kwamba limesababishwa na Metcalf, mhandisi ukarabati mstaafu.
Juzi kwenye Mahakama ya Leeds alihukumiwa kifungo cha miaka tisa jela kwa kusasababisha vifo kutokana na uendeshaji wake wa hatari, ambapo alikiri mashitaka hayo katika hatua za awali za kesi hiyo.
Akitoa hukumu, Jaji Geoffrey Marson alisema Meheohra alifanya 'makusudi kuendesha kwa kasi' na alitumia gari lake kama silaha.
Baadaye Clive Metcalf alisema: "Tumekuwa tukiambiwa kwamba ameomba radhi, lakini hatukubali kwamba hizo ni taarifa rasmi za kuomba radhi.
"Aliamua kuja nchini kinyume cha sheria; aliamua kunywa usiku mzima na kuendesha gari; aliamua kuendesha gari kwa mwendo mkali sana akivunja sheria za barabarani; aliamua kujaribu kukimbia eneo la ajali mbaya na kukana hakuwa dereva na kugomea kupimwa kama alikuwa kalewa.
"Kufuatia yote hayo, tunadhani kitu pekee anachoomba msamaha ni kwamba amekamatwa."

No comments:
Post a Comment