Mchungaji Marvin Winans, mtu aliyeongoza huduma ya mazishi ya Whitney Houston ameporwa gari lake wakati akijaza mafuta kwenye kituo kimoja cha Detroit jana.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari ambavyo havikutaka kutajwa hadharani, Winans alikuwa akijaza mafuta kwenye gari lake ndipo watekaji hao walipomvamia na kumpora mchungaji huyo mwenye miaka 54 gari lake aina ya Infiniti QX56 SUV.
Mchungaji huyo aliviambia vyombo vya habari kwamba alishaona kwamba 'haikuwa dalili nzuri' pale alipoona kundi la vijana likielekea kituoni hapo ambapo wanne kati yao wakamvamia.
Winans, ambaye familia yake ni imebobea katika muziki wa injili duniani, hakupata majeraha makubwa lakini kijana wake, Marvin Winans Jr., amesema baba yake alichekiwa hospitali na kupatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa polisi, watuhumiwa wanne walimpora Winans kiasi cha fedha ambacho hakijatajwa na kutokomea na gari lake. Wamewataja waporaji watatu kati yao kuwa ni wanaume weusi.
Winans aliongoza vema huduma ya mazishi ya Whitney mjini New Jersey Februari, mwaka huu na kupongezwa na mama wa marehemu kwa kuileta 'dunia' kanisani.

No comments:
Post a Comment