Licha ya kusisitizwa kuwa itakuwa shughuli ya faragha, imeelezwa kwamba mazishi mkongwe wa muziki Donna Summer mjini Tennessee yamehudhuriwa na nyota kibao wa muziki duniani akiwamo prodyuza mashuhuri David Foster.
Awali ilikadiriwa mazishi hayo yatahudhuriwa na waombolezaji 1,000 waliopewa mwaliko.
Licha ya kuandaa vibao kadhaa vya Donna Summer, Foster ameshiriki kikamilifu katika kutengeneza kazi za waimbaji mbalimbali maarufu duniani kama Michael Jackson, Kundi la Bee Gees, Mariah Carey, Beyonce, Prince, Madonna na wengine wengi.
Vyanzo vimeeleza, Prodyuza wa Italia Giorgio Moroder naye pia amehudhuria mazishi hayo. Moroder ametengeneza nyimbo kadhaa za Donna Summer zilizotamba zikiwamo 'Love to Love You Baby' na 'I Feel Love'.
Imeelezwa jeneza la Donna Summer lilizingirwa na maua waridi meupe. Familia nzima ya mwimbaji huyo gwiji nayo ipo kwenye mazishi hayo.
Donna Summer alifariki dunia akiwa na miaka 63, mjini Florida wiki iliyopita baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani kwa muda mrefu.

No comments:
Post a Comment