Monday, May 28, 2012

MAJESHI YA SYRIA YAUA KINYAMA WANAWAKE NA WATOTO 47...

Kwenye sakafu ya chumba, miili ya watoto wa Syria imelala kana kwamba midoli imepangwa. Macho ya baadhi yao yakiwa wazi, wakionekana kana kwamba mawindo.
Hakina aliyezidi umri wa miaka minane, binti aliyetapakaa damu akiwa amevalia kiremba kichwani na mkanda mwekundu, anatazamana usoni na kijana mdogo wa kiume.
Kuwazunguka, mamia wengine, baadhi wakiwa wamekatwa mikono wamelaliana bega kwa bega.
Hayo yote yalikuwa ni mauaji ya halaiki Ijumaa iliyopita, wanadai wanaharakati, wakati wahuni wanaomuunga mkono Rais Bashar Assad waliposafisha miji na vijiji katika eneo la katikatika ya nchi hiyo la Homs.
Wanaume inasemekana waliuawa mitaani, wakati wanawake na watoto walipigwa risasi na kuchomwa visu majumbani mwao.
Picha ambazo si rahisi kuziangalia zimepatikana kutoka kwenye filamu iliyopigwa na mtu mmoja na kutumwa kwenye mtandao.
Kwa nyuma sauti ya mtu mzima inaweza kusikika akilia: "Mungu wangu, Mungu wangu, Mungu wangu."
Wanaharakati wamesema zaidi ya watu 100 waliuawa kwenye mashambulio, kati yao 50 wanasemekana kuwa ni watoto, wengi wao wakiwa chini ya umri wa miaka 10.
Video nyingine zilizotumwa mtandaoni zinaonesha watoto waliokufa wakiwa wamefunikwa na mashuka na mablanketi. Katika moja, watoto wasiopungua 12, baadhi wakiwa na matundu vichwani mwao na usoni, wamelala katika kinachoonekana kuwa ni sakafu ya msikiti.
"Wameua familia zote, kuanzia wazazi mpaka watoto, lakini walilenga zaidi watoto," amedai mmoja wa wanaharakati. Aliongeza kwamba wakazi, wanahofia mashambulio zaidi, wakitumia siku ya jana kukimbia kutoka eneo hilo.
Shambulio baya zaidi ni Houla, kaskazini-magharibi kwa mji wa Homs, mji mkuu wa Jimbo la Homs.
Imechochewa na shambulio moja baya zaidi la umwagaji wa damu kutokea Syria katika kipindi cha mapinduzi yaliyodumu kwa miezi 15.
Wanaharakati kutoka eneo hilo wamesema vikosi vya uasi vimeshambulia Houla kufuatia maandamano makubwa ya upinzani yaliyofanyika Ijumaa iliyopita.
Wapinzani wa Syria pia wanatuhumu vikosi vya usalama kwa mauaji ya wanawake 47 na watoto kwenye mji wa Homs.
Hadi Abdallah, mwanaharakati wa Syria, amesema miili 26 ya watoto na wanawake 21, baadhi makoo yao yakinyofolewa na wengine wakiwa na majeraha makubwa, walikutwa eneo la Karm el-Zaytoun na Al-Adawiyeh na maeneo jiarani.
"Baadhi ya watoto walipigwa na vitu vigumu vichwani mwao, binti mmoja alilawitiwa na wanawake walibakwa kabla ya kuuawa," alisema.
Mji uliopo kaskazini wa Aleppo, kitovu kikuu cha uchumi wa nchi hiyo, ndio pekee uliokuwa umebaki wenye kumuunga mkono Assad katika harakati za mapinduzi, lakini nako sasa vuguvugu la uasi limeshika kasi katika wiki za hivi karibuni.
Ijumaa vikosi vya Syria vilipiga mabomu ya machozi na risasi za moto kujaribu kuwatawanya maelfu ya waandamanaji mjini Aleppo waliokuwa wakimtaka Assad aondoke madarakani, na kuua watu watano, wanaharakati wamesema.

No comments: