Sunday, May 13, 2012

KIPINDI KIPYA KUMTOA KIMUZIKI MTOTO WA WHITNEY...



Mama wa mwimbaji Whitney Houston amewaeleza marafiki zake ameunga mkono wazo la kuanzishwa kipindi cha televisheni kuhusu familia hiyo sababu anaamini itakuwa nafasi nzuri kwa Bobbi Kristina kutimiza ndoto zake za uimbaji.
Vyanzo vya habari vilivyo jirani na familia ya Houston vimesema, mama huyo Cissy anajua kwamba Bobbi amerithi kipaji cha mama yake cha uimbaji, hivyo anaamini katika kipindi hicho itakuwa sehemu muafaka kwa Bobbi kuonesha kipaji chake.
Imeelezwa kwamba Cissy pia anaamini kipindi hicho, 'kitasaidia mchakato wa uponyaji' kwa 'kuwafanya wanafamilia kuwa kitu kimoja.'
Pia Cissy amefurahia ukweli kwamba 'familia hiyo pana' itaingiza fedha kutokana na mkataba huo.
Wakati huohuo, habari zilizopatikana baadaye zinadai kuwa ukimya wa Bobby Brown ambaye ni baba wa Bobbi Kristina umetokana na  kwamba baba huyo alikuwa akimuwinda binti yake huyo kwa ajili ya kipindi chake kipya cha televisheni kinachofanana na hiki cha familia ya Houston.
Imeelezwa kwamba kwa miezi kadhaa Bobby amekuwa akilazimika kumtumia Pati Houston ili kumshawishi bila mafanikio Bobbi Kristina ambaye amemkatia 'laini' zote baba huyo kwa sasa.
Familia ya Houston inaamini kwamba Bobby Brown anataka kumtumia binti yake Bobbi kukipatia umaarufu kipindi chake hicho anachotarajia kukirusha hewani siku za hivi karibuni.

No comments: