Mwimbaji Jennifer Hudson ameibuka maarufu miongoni mwa wajumbe wa Baraza la Wazee wa Mahakama linalosikiliza kesi ya mauaji inayomkabili William Balfour, kufuatia utafiti kuonesha kuwa kila mjumbe kati yao alikiri kumfahamu nyota huyo kabla ya kesi hiyo kuanza.
Fomu za maoni zilisambazwa na kujazwa na wajumbe wote walioshiriki baraza hilo kabla ya kuanza kikao cha kuamua hatia ya William katika tuhuma za kuua familia ya Jennifer Hudson.
Kati ya wajumbe 12 hadi 15 walikiri kumfahamu Jennifer tangu mdogo wakati akianza shughuli zake za muziki, huku sita wakianza kumfahamu wakati aliposhiriki shindano la 'American Idol.'
Mjumbe pekee ambaye hakuwahi kumuona Jennifer kwenye 'Tuzo za Oscar' wala 'Idol' alisema amemfahamu nyota huyo kupitia kwenye televisheni lakini alishindwa kubainisha ni katika kipindi kipi hasa cha runinga.
Mmoja wa magwiji wa sheria alisema kuwa kiwango cha umaarufu wa Jennifer hakiathiri maamuzi katika kesi inayomkabili Balfour sababu ni kawaida kwa wajumbe wa baraza kuwatambua watu maarufu.
Pia haimaanishi kutokana na umaarufu huo basi kutamfanya Balfour aonekane kuwa na hatia zaidi.
William Balfour anakabiliwa na kifungo cha maisha jela baada ya kutiwa hatiani kwa mauaji ya familia ya Jennifer akiwamo mama, kaka na mtoto wa dada yake na hukumu inatarajiwa kutolewa hivi karibuni.

1 comment:
Great blog here! Also your web site loads up fast! What host are you using?
Can I get your affiliate link to your host? I wish my web site loaded up as quickly as yours lol
My site: mackeeper 05
Post a Comment