HAKUNA KAMA JOSE MOURINHO ULAYA...
Kocha Jose Mourinho ameiongoza timu ya Real Madrid kutwaa ubingwa wake wa kwanza wa Ligi ya Hispania 'La Liga' tangu mwaka 2008.
Mourinho ameweka rekodi mpya ya kuwa kocha wa kwanza kuweza kutwaa ubingwa katika nchi nne tofauti Ulaya akiwa na timu tofauti. Kabla ya Real Madrid, Mourinho alifanya hivyo kwa timu za FC Porto ya Ureno, Chelsea ya England na Inter Milan ya Italia.

No comments:
Post a Comment