Monday, May 21, 2012

DAMILIA YA WHITNEY YAINGIA KWENYE MZOZO MWINGINE...

Familia ya Whitney Houston imejikuta kwenye mzozo mwingine safari hii ikiwa ni kuhusiana na Tuzo za Muziki za Billboard/
Wakati wifi wa Whitney, Pat Houston akifanya kila linalowezekana aweze kwenda kupokea tuzo kwa niaba ya Whitney, binti wa mwimbaji huyo wa zamani, Bobbi Kristina naye anajiona kuwa ndiye anayestahili kufanya hivyo.
Vyanzo vya habari vimesema kuwa Pat analazimisha kwenda kupokea tuzo hizo za Milenia kwenye sherehe zilizotarajiwa kufanyika mjini Las Vegas usiku wa kuamkia leo kinyume na matakwa ya waandaji wa tuzo hizo.
Imeelezwa kwamba waandaji wa tuzo hizo wanataka Bobbi Kristina ndiye apokee tuzo hiyo na kutoa hotuba fupi kwa niaba ya mama yake, jambo ambalo Pat anapingana nalo kwa nguvu zote hali inayozidi kuleta mtafaruku kati yake na Bobbi.
Vyanzo vya habari vimesema, waandaaji wanaona Bobbi ndilo chaguo sahihi kumwakilisha mama yake Whitney na kwamba jitihada za Pat wanaziona kama ni kujitafutia umaarufu tu kwa ajili ya kipindi chake kijacho cha televisheni.

No comments: