Mume na mke baada ya kuishi kwa miaka kadhaa, wakapanga wikiendi moja kujikumbushia maisha yao kabla hawajaoana. Wakakubaliana wajikumbushie matukio wakati wakianza ufariki wao. Siku ya siku, mume akatoka na kwenda kama mita mia moja kutoka nyumbani na kumtaka mkewe amfuate huko wakati wa usiku majira ya waa tatu. Baada ya kusubiri hadi usiku wa manane bila mke kutokea eneo walilokubaliana, mume akaamua kurejea nyumbani kwa hasira na kumvamia mkewe, "Wewe tumekubaliana nini na ukafanya nini tena? Mke kwa upole akajibu, "Wazazi walinizuia nisitoke usiku!" Duh, balaa...

No comments:
Post a Comment