Monday, May 21, 2012

CHEKA TARATIBU...

Jamaa watatu wamekufa kwenye ajali ya gari na moja kwa moja wanakutana na Yesu. Akawaambia, "Sasa nawauliza swali moja rahisi kila mmoja. Ukiniambia ukweli utaingia peponi lakini ukinidanganya basi utaenda motoni.
Akamuuliza wa kwanza, "Ni mara ngapi umetembea nje ya ndoa?" Akajibu, "Mara zote nimekuwa mume mwaminifu." Yesu akasema, "Safi sana. Sasa sio tu kwamba nakuruhusu kuingia peponi bali nitakupa jumba kubwa na Range Rover."
Yesu akamuuliza wa pili, "Ni mara ngapi umetembea nje ya ndoa?" Jamaa akajibu, "Nimetembea nje ya ndoa mara mbili." Yesu akajibu, "Ninakupa nafasi ya kuingia peponi, lakini kutokana na kukosa uaminifu kwenye ndoa nitakupa nyumba ya vyumba vinne na Toyota Corolla la kutembelea.
Yesu akamuuliza wa tatu, "Ni mara ngapi umetembea nje ya ndoa?" Jamaa akajibu, "Kama mara nane hivi." Yesu akajibu, "Nawe nakuruhusu kuingia peponi. Lakini kutokana na kukosa kwako uaminifu nakupatia chumba kimoja na Bodaboda."
Masaa kadhaa baadaye jamaa wa pili na wa tatu wakamwona mwenzao wa kwana akilia kwa uchungu. Wakamuuliza, "Unalia nini wakati umepewa jumba kubwa na Range Rover? Jamaa wa kwanza akawajibu, "Ninalia sababu muda mfupi uliopita nimemuona mke wangu akiendesha baiskeli huku usiku akilala nje!" Duh, chemsha akili...

No comments: