Mzee mmoja kutoka mikoa ya Kusini kwa mara ya kwanza yuko safarini kuja Dar es Salaam. Akiwa kwenye basi, kwa muda mrefu macho yake yalikuwa kwa dereva anavyobadilisha gia. Basi bwana ikafika wakati basi likasimama na abiria wote wakatakiwa kushuka kwenda kujipatia chochote cha kula. Hapo ndipo yule mzee akainuka na kwenda moja kwa moja sehemu ya dereva ambaye wakati huo alikuwa kashuka. Kwa dakika kama kumi yule mzee akawa tayari amefanikiwa kung'oa gia. Wakati safari ikitaka kuanza, dereva akagundua gia haikuwapo mahali pake na kuuliza kwa sauti. Yule mzee bila wasiwasi akajibu, "Tangia Ntwala (Mtwara) mi kukuona tu kuhangaika kutoa. Mi kutoa dakika mbili tu njomba!" Duh...

No comments:
Post a Comment