Friday, May 18, 2012

CHEKA TARATIBU...

Mwanasheria maarufu jijini amefariki na kuwasili kwenye milango ya mbinguni. Mtakatifu Petro akamuuliza, "Umefanya nini cha maana kukuwezesha kuingia Peponi?" Mwanasheria akafikiria kwa muda na kujibu, "Wiki iliyopita nimegawa nusu ya kipato changu kwa watoto wa mitaani." Petro akamwambia Malaika Gabriel kutazama kwenye kitabu cha kumbukumbu, na baada ya muda Gabriel akathibitisha kuwa ni kweli. Petro akasema, "Vema, lakini hiyo haitoshi kukuingiza Peponi." Mwanasheria akasema, "Ngoja, Ngoja! Kuna vingine zaidi! Miaka mitatu iliyopita niliwapatia wasiojiweza nusu ya kipato changu." Mtakatifu Petro akamtuma Gabriel kucheki na akathibitisha kwamba ni kweli. Mtakatifu Petro akamuuliza Gabriel, "Vema, unashauri tumfanye nini kwa huyu jamaa?" Malaika Gabriel akamgeukiwa Petro na kusema, "Wacha tumrudishie laki mbili zake halafu tumpeleke jehanamu!" Duh, kuweni makini na mnachomtolea Mungu...

No comments: