Mume kafika nyumbani kutoka kazini akiwa mnyonge. Mke akamuuliza kulikoni? Mume akajibu, "Jengo la ofisi zetu limeteketea moto na wenzangu wote wamekufa." Mke akadakia, "Duh, pole sana. Sasa wewe umenusurika vipi?" Mume akajibu, "Nilienda kununua sigara nje ya jengo." Mke akaendelea, "Masikini, sijui familia zao wataishi vipi?" Mume akajibu, "Watalipwa bima milioni 20 kila familia." Duh, mke kusikia hivyo akafoka kwa sauti, "Umeona sasa misigara yako hiyo, tumekosa hivihivi mamilioni!"

No comments:
Post a Comment