Mlevi mmoja kaingia kwenye baa moja jirani na maeneo ya Ubungo Darajani. Baada ya kunywa bia kadhaa, mhudumu akamfuata kudai bili yake, "Mzee, nakudai elfu tisa!" Yule mlevi kwa kujiamini akajibu, "Nimeshakulipa wewe!" Baada ya kufikiri kwa sekunde kadhaa mhudumu akajibu, "Kama unasema umelipa, poa!" Mlevi akatoka nje na kukutana na mlevi mwenzake. "Oyaa mshikaji, ingia baa hii mhudumu hana kumbukumbuku kabisaaa," yule mlevi akamweleza rafiki yake. Mlevi wa pili baada ya kunywa na kudaiwa bili, akajibu vilevile kama alivyoelezwa na mwenzake. Mhudumu akakubali na yule mlevi akaishia zake. Njiani akakutana na mlevi mwenzake na kumpa ujanja kama ule. Mlevi wa tatu alipoingia baa na kunywa karibu kreti mhudumu akasimama kando yake na kusema, "Unajua bro, leo kuna maajabu yametokea hapa baa. Walevi wawili wameingia hapa na kudai kuwa wameshanilipa. Sasa nasubiri mlevi atayefuatia kusema hivyo nimshindilie magumi ya ukweli!" Yule mlevi kusikia vile akasema huku akinyanyuka, "Duh, kama umeamua hivyo basi nipe chenji yangu kabisaa niondoke!" Ama kweli mjini shule...

No comments:
Post a Comment