Vijana kadhaa wamekwenda kwenye majaribio kwa ajili ya kuingia Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ). Wakiwa wamechanganyika makabila mbalimbali, wakashangaa majibu ya majaribio yakiwatupa nje wengine wote isipokuwa waliokuwa wametokea mkoa wa Mara. Ndipo kijana mmoja akaingiwa na ujasiri na kwenda kwa mkuu wa mafunzo hayo na kuhoji, "Afande, imekuwaje makabila mengine wote tushindwe ukawapitisha wenyeji wa Mara?" Afande akacheka kidogo na kumjibu, "Hii ni JWTZ, yaani Jeshi la Wakurya Tangu Zamani!" ...Upo hapo?

No comments:
Post a Comment