Rubani mmoja kaamua kumsaidia dada mmoja ambaye ilikuwa mara yake ya kwanza kutumia usafiri wa ndege. Kwa kuwa safari hiyo ilikuwa ikiunganisha mashirika kadhaa tofauti ya ndege, ikalazimika abiria kulala nchi moja kusubiri ndege ya kuunganisha huko waendako. Rubani akampeleka jamaa hotelini na kuhakikisha amepata chumba kisha yeye kuondoka. Kesho yake abiria wote wakiwa tayari kwenye ndege, rubani akagundua yule jamaa hayumo mle ndani hivyo akapiga simu hotelini kujua kulikoni? Rubani: "Aisee vipi mbona sikuoni?" Jamaa: "Nimekwama chumbani, siwezi kutoka." Rubani: "Kwa vipi?" Jamaa: "Kuna milango mitatu sijui nipite upi kutoka nje. Mmoja ni wa jikoni, wa pili ni bafuni na huu wa tatu umeandikwa 'Do Not Disturb!" Duh...

No comments:
Post a Comment