KUTOKA KUSHOTO: Wazazi wa Eliott. KATIKATI: Emily enzi za uhai wake (juu) na akiwa na Eliott (chini). KULIA: Nyumba alimofia Emily (juu) na akiwa na mama yake (chini).
Mtoto wa sonara tajiri amemshambulia rafiki yake wa kike kitandani kufuatia wivu wa kimapenzi nyumbani kwa wazazi wake kabla wazazi hao kumsaidia kumuua, imeelezwa mahakamani.
Eliott Turner mwenye miaka 20 anatuhumiwa kumuua Emily Longley mwenye miaka 17 baada ya kuhisi kuwa msichana huyo ana mahusiano ya kimapenzi na mtu mwingine ndani ya urafiki wao huo uliodumu kwa miezi minne tu.
Eliott anasemekana mara kwa mara alikuwa akitishia kumuua Emily kwa kumtwanga na nyundo akijigamba: "Nitakwenda gerezani kwa ajili hiyo na nitabaki kuwa milionea nikitoka."
Mahakama Kuu ya Winchester ilielezwa kwamba baada ya kufanya mauaji hayo Mei 7 mwaka jana, Eliott aliandika waraka kuungama makosa yake lakini waraka huo ulichanwa na baba yake, Leigh. Wazee wa mahakama waliwaeleza polisi nyumbani kwa familia hiyo Bournemouth kwamba familia hiyo 'iliteketeza ushahidi wote na kuwadanganya polisi'.
Mama yake, Anita mwenye miaka 51, na baba, Leigh mwenye miaka 57 wa Bournemouth, mwanzoni waliwaeleza polisi kwamba walimsikia Emily akizungumza ndani ya chumba cha kijana wao, licha ya kwamba waendesha mashitaka walisema kwamba alishakufa.
Eliott alisema walikuwa wakilumbana siku moja kabla ya kumshambulia na alipoamka kando yake alikuwa amekufa.
Alipokamatwa alikuwa na pasi yake ya kusafiria mfukoni na begi lenye nguo zake, Mahakama Kuu ya Winchester ilielezwa.
Leigh na Anita wanadaiwa kuondoa koti la kijana wao chumbani wakati polisis walipozuiliwa na Leigh alipoangusha vidonge sakafuni na Anita kulishikilia.
Katika ushahidi uliosomwa mahakamani, Leigh anadaiwa kuhanikiza kwa kusema: "Eliott mnyongelee mbali huyo."
Mahakama pia ilielezwa kuwa Leigh alisema: "Siwezi kuwaambia polisi kuhusu waraka niliouchana akisema Eliott alimuua Emily lakini hakudhamiria kufanya hivyo."
Kesi hiyo inaendelea.

No comments:
Post a Comment