Daktari wa meno amemng'oa meno yote rafiki yake wa kiume aliyemtosa na kuanzisha mahusiano na mwanamke mwingine, ambaye naye pia kamwacha mwanaume huyo kwa kuwa sasa ni kibogoyo.
Anna Mackowiak mwenye miaka 34, anakabiliwa na adhabu ya kifungo jela kwa kumlipizia Marek Olszewski mwenye miaka 45 alipokwenda kung'oa jino siku chache baada ya kuvunja mahusiano na daktari huyo.
Alimpatia dozi kubwa ya ganzi na kukwanyua meno yote mdomoni.
Kisha daktari huyo akamjaza pamba mdomoni na kumweleza kuwa ana matatizo makubwa hivyo anatakiwa akamwone daktari bingwa.
Daktari huyo wa meno anayefanya kazi mjini Wroclaw, Poland alisema: "Nilijaribu sana kuzingatia taaluma yangu na kuondoa hisia zangu binafsi.
"Lakini nilipomwona kajilaza kitandani, ndipo mawazo yakabadilika."
Olszewski anasema: "Nilijua kuna kitu kibaya kimetokea sababu nilipoamka sikuhisi meno na mdomoni kulijazwa pamba.
"Aliniambia mdomo wangu una ganzi na kwamba sitaweza kuhisi chochote kwa kipindi fulani na kwamba pamba hizo mdomoni ameweka kwa ajili ya kukinga fizi zangu, lakini nahitaji kuonana na daktari bingwa.
"Sikuwa na sababu zozote za kumhofia, namaanisha niliamini anazingatia maadili ya taaluma yake.
"Lakini nilipofika nyumbani nilitazama kwenye kioo sikuweza kuamini macho yangu. Yule mwanamke alisafisha kila kitu mdomoni.
"Rafiki yangu mpya wa kike naye kanikimbia akisema hawezi kuwa na mwanaume asiye na meno.
"Na ninatakiwa kugharimia meno bandia ama kitu fulani."
Anna anachunguzwa kwa kukiuka maadili ya taaluma yake na kumdhalilisha mgonjwa aliyemuamini. Anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani.

No comments:
Post a Comment