Friday, May 25, 2012

AMBER PORTWOOD AOMBA JAJI AMFUNGE MIAKA MITANO JELA...

Mwigizaji maarufu Amber Portwood amefungwa pingu na kupelekwa rumande juzi baada ya kumtaka jaji kumfunga jela huku picha zake za mwisho zikizagaa mitaani.
Amber hakuonesha hisia zozote wakati akielekea kwenye chumba cha mahakama ya Indiana ambako shauri lake kuhusu matumizi ya dawa za kulevya limekuwa likisikilizwa kwa wiki sasa na imeelezwa amebwaga manyanga katika harakati hizo za kujaribu kumrekebisha tabia.
Amber alimweleza Jaji kwamba hakuwahi kujirekebisha tangu alipohukumiwa kuhudhuria mpango wa ushauri nasaha mara baada ya kukamatwa akitumia dawa hizo Desemba mwaka jana. Tangu kipindi hicho amekiri kuwa 'msichana mbaya' hivyo ni bora angefungwa miaka mitano jela ambayo kwa kawaida Jaji angepaswa kumhukumu.
Ilishitusha sana, lakini Amber akamwacha Jaji hana la kufanya bali kuamuru awekwe rumande.
Amber abaki rumande hadi hukumu yake itakapotolewa wiki chache zijazo.

No comments: