Sunday, April 22, 2012

WALIOBAKA WAKISHEREHEKEA SIKUKUU YA IDD WAFUNGWA MIAKA 38 JELA...

Kundi la vijana wa Kiislamu ambalo liliwatorosha na kuwabaka wasichana wawili walio chini ya miaka 20 kama sehemu ya sherehe za Sikukuu ya Idd wameangua kicheko mahakamani juzi wakati wakihukumiwa kifungo cha jumla ya miaka 38 jela.
Wasichana hao, mmoja mwenye miaka 15 na mwingine miaka 16, walipelekwa maili kadhaa kutoka majumbani kwao hadi kwenye hosteli iliyoko mafichoni.
Katika wikiendi hiyo ya kutisha, walinyweshwa pombe na kubakwa na wanaume wawili, Shamrez Rashid na Amar Hussein kwa kurudia rudia, kabla ya kukabidhiwa kwa wanaume wengine ambao pia 'waliwatumia kufanya nao ngono'.
Msichana mwenye miaka 16 yeye alilazimishwa kufanya ngono mara sita na wanaume wanne tofauti.
Msichana mdogo alibakwa na mwanaume mmoja na kudhalilishwa na wengine waliobaki.
Mmoja wa watuhumiwa hao, Rashid mwenye miaka 20, alidaiwa kusema kuwa wasichana hao walifurahia kitendo hicho, ambachi amedai kilifanyika wakati wakisherehekea sikukuu ya Kiislamu ya Idd.
"Ilikuwa Idd," alisema. "Tuliwakaribisha kama wageni wetu. Sawa, wakaturuhusu kufanya nao ngono lakini tulikuwa tukiwanunulia chakula na vinywaji.
"Walipata kila walichotaka. Waliburudika."
Mwenzake, Amar Hussain mwenye miaka 22 alidai wasichana hao walikuwa machangudoa.
Lakini Jaji Melbourne Inman QC alisema wasichana hao walikuwa bado watoto wakati wakifanyiwa unyama huo.
Alisema ilikuwa kawaida kabisa kwamba walifuatana na wanaume, lakini hili halihusiani na tabia za wabakaji hao.
"Walikuwa hawajitambui kabisa na mkatumia nafasi hiyo."
Washitakiwa watano waliangua kicheko wakati matendo yao ya kinyama yakisomwa mahakamani hapo jana.
Rashid ambaye tayari alitiwa hatiani kwa makosa mawili ubakaji, kujaribu kubaka, utoroshaji mtoto na kujaribu kudhalilisha mwili, aliangua kicheko akiwa kwenye kizimba.
Mahakama ilisikia jinsi Rashid na Hussain walivyowatorosha wasichana kutoka kwao Telford mjini Shropshire hadi Birmingham kwenye hosteli ya muda jioni ya Jumamosi Novemba 28, 2009.
Waliwapeleka kwenye sehemu wasiyoifahamu kusudi watulie na kuwatii kwa kila watakachowaamuru," mwendesha mashitaka alisema.
Baada ya kumaliza kuwabaka, 'wakawatoa kwa marafiki zao msururu wa vijana ndani ya nyumba.'
Zaidi ya masaa 36 yaliyofuatia, wasichana hao walikabiliana na udhalilishaji licha ya kujaribu kuwazuia wabakaji hao bila mafanikio.
Mahakama Kuu ya mjini Birmingham imekuwa ikipokea keshi nyingi ambapo vikundi vya vijana wamekuwa wakidaiwa kulazimisha kufanya ngono na wasichana.
Hussain alipatikana na hatia ya udhalilishaji watoto na makosa matatu ya ubakaji hivyo akahukumiwa kifungo cha miaka 11 jela.
Rashid alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa makosa mawili ya ubakaji, kudhalilisha watoto na kujaribu kufanya udhalilishaji wa kijinsia.
Adil Saleem mwenye miaka 20, alihukumiwa miaka nane jela kwa kosa moja la kubaka. Jahbar Rafiq mwenye miaka 28 naye alihukumiwa kifungo cha miaka nane kwa ubakaji na udhalilishaji na Amer Islam Choudhrey mwenye miaka 20 alihukumiwa kifungo cha miezi 15 kwa makosa ya udhalilishaji watoto na udhalilishaji kijinsia.

No comments: