MKONGWE ALIYEMUDU KUENDESHA KIPINDI MIAKA 38 AFARIKI DUNIA...

Mtangazaji maarufu ambaye ametamba na kipindi chake cha televisheni "60 Minutes" kwa miaka 38 kabla ya kustaafu mwaka 2006, Mike Wallace amefariki dunia jana akiwa na umri wa miaka.
Bob Scheiffer, mwendeshaji wa kipindi cha "Face the Nation," alitangaza kifo hicho kwenye televisheni ya CBS jana asubuhi akisema kwamba Wallace alifariki Jumamosi usiku mjini New Haven huku akiwa amezungukwa na familia yake.
Afya ya Wallace ilikuwa ikizorota siku hadi siku katika miaka ya hivi karibuni.
Mahojiano yake ya mwisho kwenye televisheni ya CBS ni yale aliyomhoji mchezaji nyota wa zamani wa soka la Kimarekani (Baseball), Roger Clemens, ambayo yalirushwa Januari, 2008.
Wallace alikuwa mtu wa kwanza kuazimwa na prodyuza mkongwe wa CBS, Don Hewitt wakati akiunda timu ya kuendesha kipindi cha "60 Minutes."
Katika historia yake, Wallace ameshinda Tuzo 21 za Emmy, Tuzo tano za Waandishi za DuPont-Columbia, na Tuzo tano za Peabody.
Wallace hakuwa na tatizo katika kuwakabili wageni wake kwenye kipindi chake na mifano bora miwili ni mahojiano aliyofanya na Barbra Streisand mwaka 1991 na Louis Farrakhan mwaka 2005.

No comments: