Saturday, April 21, 2012

JUMBA LILILOANGUKIWA NA NDEGE MWAKA 1946 LAPIGWA BEI...



Inauzwa...Hekalu la kuvutia lililoko Beverly Hills lenye ukubwa wa futi za mraba 6,246 pamoja na bwawa la kuogelea ambalo zamani liliwahi kuangukiwa na ndege ya Howard Hughes na kuharibiwa vibaya eneo la gereji. Kwa mujibu wa marafiki wa mtandao wa curbed.com, hekalu hilo linalomilikiwa na mwigizaji Rosemary DeCamp liliingia sokoni kwa bei ya Dola za Marekani milioni 6.9. Ni moja ya nyumba ambazo ziliangukiwa na kuharibiwa vibaya baada ya ndege ya Hughes XF-11 kuanguka Beverly Hill Julai 11, 1946 kufuatia Hughes aliyekuwa akiiendesha kuishiwa mafuta angani. Hughes aligonga nyumba tatu wakati akiwa katika harakati za kutua likiwamo hekalu hili Namba 805 N. Linden. Hughes alitumbukia kwenye paa la chumbani na kuserereka hadi gereji, kabla mwishoni kujikita kwenye nyumba nyingine ya jirani. Hughes alijeruhiwa vibaya kwenye ajali hiyo...ambayo baadaye ilitengenezewa sinema, "Aviator."

No comments: