Thursday, April 19, 2012

GWIJI WA BURUDANI DICK CKARK AFARIKI DUNIA....


    BREAKING NEWS!!   
Prodyuza maarufu wa kipindi cha televisheni cha "New Year's Rockin' Eve" amefariki asubuhi hii kutokana na maradhi ya moyo akiwa na umri wa miaka 82.
Mwakilishi wa Clark amesema nyota huyo wa televisheni alikuwa amekwenda kwenye hospitali ya St. John mjini Los Angeles kwa matibabu ya kawaida jana usiku. Clark alipatwa na mshituko mkubwa wa moyo wakati akiendelea na utaratibu wa kupata matibabu hospitalini hapo. Juhudi za kuokoa maisha yake zilishindikana.
Gwiji huyo ataagwa leo nje ya Jumba la Burudani aliloliasisi lililoko Branson, mjini Missouri.
Msemaji wa Jumba hilo alisema, wafanyakazi pamoja na mashabiki watakujikusanya pamoja nje ya jumba hilo leo na kufanya onesho maalumu kwa ajili ya kumuenzi gwiji huyo wa burudani.
Imeelezwa kuwa watu wamelitoa onesho hilo la leo kama fursa ya kuyaenzi maisha ya gwiji huyo.
Clark alifungua rasmi Jumba hilo mwaka 2006 na kupata umaarufu mkubwa sana duniani.

No comments: