Mshamba mmoja kutoka kijijini kaingia Dar kwa mara ya kwanza na kiroba chake kwapani. Baada tu ya kutoka Stendi Kuu ya Mabasi ya Mikoani pale Ubungo si akaamua kujisaidia kando ya barabara. Mara akatokea askari wa doria na kumkamata kwakuwa ni kosa kujisaidia hadharani. Bila kuchelewa yule askari akamtaka yule mshamba atoe 10,000 ili amwachie. Baada ya mshamba yule kusema hana, ndipo askari akamtandika kirungu cha mgongo na kusema, "Hii ndio chai yako!" Yule mshamba akainama chini akiugulia maumivu huku askari akiwa anasubiria ainuke. Punde mshamba akainuka na kwa mshangao akamjibu askari kwa unyenyekevu, "Asante nashukuru kwa chai!" Wakati askari akitabasamu kusikia jibu hilo, akashtukia bonge la konde likitua usoni mwake na kumpeleka chini huku likifuatiwa na maneno, "Chai ilikuwa tamu shika kikombe chako!" Kha....

No comments:
Post a Comment