Katika moja ya safari zake huko Vatican, siku moja Baba Mtakatifu Papa Benedict XVI kaamua kumpumzisha dereva wake na kuendesha gari huku dereva akiwa amejilaza kiti cha pembeni. Wakiwa njiani wakasimamishwa na askari wa usalama na kuombwa wajitambulishe. "Naitwa Papa Benedict," akaanza kujitambulisha. Duh! Kwa mshangao askari kusikia hivyo akatimua mbio huku akijisemea mwenyewe, "Kama Baba Mtakatifu ndio dereva, yule kiti cha pembeni lazima atakuwa Yesu..! Kha, woga mwingine bwana...

No comments:
Post a Comment