CHEKA TARATIBU...

Jamaa watatu wako kwenye ndege ndogo kutoka Kigoma kwenda Arusha. Rubani alikuwa Paroko na abiria wake wawili ambao ni mwalimu wa dini na mwanafunzi wake. Wakiwa katikati ya safari, ndege ikapata hitilafu angani hivyo kutakiwa kuruka. Paroko akawaambia abiria wake wavae majaketi ya kuokolea maisha na kuruka nje. Kwa bahati mbaya majaketi yalikuwa mawili tu, na haraka mwalimu akavaa chapchap bila kungoja akaruka zake nje. Mwanafunzi kwa upole akamfuata Paroko na kumwambia kulikuwa na majaketi mawili na kwamba mwalimu kachukua moja na kesharuka nje. Paroko akamwambia yule mtoto achukue lililobaki aruke nje kwakuwa ni taifa la kesho na amwache yeye afe sababu kwanza ni mzee sana. Mtoto kwa unyonge akarudi nyuma kwenye ndege huku akilia. Akavaa jaketi na kutaka kuchukua begi lake la mgongoni lililokuwa na nguo zake ili aruke nje. Shabash! Hakuliona, na badala yake alichokiona mbele yake ni jaketi lingine. Kumbe bwana katika haraka zake, mwalimu alivaa begi badala ya jaketi...Tumwombee apone!

No comments: